MakinikiA
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 5,104
- 6,827
Paul-Henri Sandaogo Damiba: Kanali wa jeshi aliyeongoza mapinduzi Burkina Faso
CHANZO CHA PICHA, ANADOLU AGENCY: Wanajeshi walioongoza mapinduzi Burkina Faso
Paul-Henri Sandaogo Damiba ndio kiongozi wa vuguvugu la Patriotic Movement for Safeguarding and Restoration (MPSR).
Siku ya Jumatatu wanajeshi wanaoshirikishwa na vuguvugu hilo walitangaza katika runinga ya kitaifa nchini humo kwamba , walimaliza utawala wa rais Roch Marc Chrisitian Kabore.
Luteni kanali Paul - Henri Sandaogo Damiba , mwenye umri wa miaka 41 ni afisa mkuu wa jeshi nchini Burkina faso.
Aliteuliwa kuchukua wadhfa huo na rais Roch Marc Christian Kabore siku moja baada ya shambulio, tarehe 14 Novemba 2021 lililotekelezwa na Wana jihad katika eneo la Inata na ambalo lilisababisha vifo vya watu 57.
Paul-Henri Sandaogo Damiba
Lakini Je kanalii huyu aliyefanikiwa kumuondoa madarakani Rais Kabore ni mtu wa aina gani?
Awali aliwahi kuhudumu kama kamanda wa kikosi cha tatu cha jeshi kinachosimamia mji mkuu wa Ouagadougou.
Kanali Damiba ni mwanajeshi wa zamani wa kikosi cha usalama wa rais, mlinzi wa zamani wa rais Blaise Campaore .
Mwaka 2015, alikuwa mmoja wa maafisa aliyepinga mapinduzi yaliofanywa na baadhi ya maafisa wa serikali yake ambayo ilivunjwa.
Aliitwa kama shahidi katika kesi iliofuata baada ya kuwasiliana na jenerali Djibril Bassole.
Tangu 2016, amekuwa katika mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi.
Alishiriki katika karibia kila operesheni, akivifunza vikosi maalum. Pia amechapisha kitabu kwa jina: Majeshi ya magharibi na ugaidi.
Paul-Henri Damiba alikuwa kiongozi wa vikosi vya jeshi vilivyokuwa katika maeneo tofauti ikiwemo Dori na Ouahigouya, eneo linalokumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara