- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwepo na chapisho linalosambaa kwenye mtandao wa Facebook likimuonesha Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame, akipiga magoti mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wakati wa ziara yake ya siku moja nchini Tanzania.
Je ?ni upi uhalisia wa chapisho hilo la picha ambalo lina sambaa kwa kasi kwenye mitando ya kigiditali..
Je ?ni upi uhalisia wa chapisho hilo la picha ambalo lina sambaa kwa kasi kwenye mitando ya kigiditali..
- Tunachokijua
- Mei 3, 2026 Rais wa Rwanda Paul Kagame alifanya ziara ya kikazi nchini Tanzania na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia SUluhu Hassan.
Madai
Kumekuwa na picha inayosambaa mtandaoni ikimuonesha Rais Kaagame akiwa amempigia magoti Rais Samia baada ya kumpokea.
Uhalisa wa Picha hiyo
Baada ya ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kidigitali ikiwemo Google reverse image search imeabainika kuwa picha hiyo imehaririwa kwa kutumia nyenzo za kidigitali.
Picha hiyo imehaririwa kutoka katika picha halisi iliyopigwa mwaka 2023 ambapo Rais Kagame alikuja Tanzania na kupokelewa katika Ikulu ya Dar es salaam. Picha hiyo ilichapishwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo ukurasa wa X wa Ikulu ya Rwanda, tazama hapa.
Picha Halisi Kutoka ukurasa wa Ikulu ya Rwanda Aprili 27, 2023
Hivyo picha hiyo si halisi lakini pia haijahaririwa kutoka katika ya mapokezi ya Rais Kagame jijini Dar es salaam.