Paul Kagame: Mapinduzi yanaweza kutokea zaidi Afrika Gen-Z wanataka mabadiliko

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amesema bara la Afrika linaweza kushuhudia mapinduzi zaidi, hasa kutokana na mtindo wa vijana wa kizazi kipya, maarufu kama Gen Z kuonyesha nia ya kupindua tawala ambazo hazitekelezi matakwa ya wananchi.

Akizungumza kufuatia mfululizo wa mapinduzi barani Afrika, ikiwemo Madagascar mwezi uliopita na machafuko ya kijeshi Guinea-Bissau wiki hii, Kagame amesema ni muhimu viongozi wa Afrika “kujiuliza sababu za mapinduzi haya badala ya kushangazwa nayo.”

Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa, tangu mwaka 1952 kumetokea mapinduzi 130 katika nchi 36 barani Afrika, huku karibu mapinduzi 10 yakitokea ndani ya miaka mitano iliyopita pekee.

Kagame amesema mataifa mengi ya Afrika, ikiwemo Rwanda, yana matatizo katika namna yanavyoendeshwa, jambo linalochochea misuguano kati ya watawala na wananchi. “Namna viongozi wanavyoendesha nchi zao inaweza kujenga mazingira ya mapinduzi,” amesema, akisisitiza kuwa vijana wanafanya hivyo wakiamini wanatafuta mabadiliko ya kiutawala na kiuchumi.

Ameongeza kuwa suluhisho si kuwadhibiti vijana, bali ni kujenga mifumo yenye uwajibikaji, haki, na kusikiliza kilio cha wananchi, hasa vizazi vipya vinavyotumia teknolojia na mitandao ya kijamii kuhamasisha hoja zao.
1764319043730.png
Chanzo: Mwanahalisi
 
Mbona kagame anaongea huku anaingalia tanzania huyu mjuba? Kaitupia jiwe tanzania kimtindo! Yeye mwenyewe tu wananchi wake wana usongo naye, ni dikteta mkomavu. Aombe sana dua gez wake wasisanuke hakuna rangi ataacha kuona
Kakosea nini kuongea hivyo..
 
Kagame katuzungumzia sisi sema kafunika sana na majani kuzungumzia sijui Guinea Bisau ni mfano tu sema kafunikia hapo kwamba vijana wasikilizwe wasitumie sana nguvu ambazo hazisaidii..
 
Mbona kagame anaongea huku anaingalia tanzania huyu mjuba? Kaitupia jiwe tanzania kimtindo! Yeye mwenyewe tu wananchi wake wana usongo naye, ni dikteta mkomavu. Aombe sana dua gez wake wasisanuke hakuna rangi ataacha kuona
Amini Nakuambia Kagame anajali Sana wananchi wake hasa vijana.
Haoendi ubadhirifu wa malinza umma.
Huduma bora za jamii.
Dikteta kweli Ila anapendwa kwa sababu hizo juu.
Jiulize udikteta wote wa Magufuli hakuna watu waliandamana Kama MO29. Hiyo ni kusema alikubakika na wananchi wengi. Waliona uadikifu na u haoakazi wake, na ufuatiliaji wa walio chini yake.
 
Ameongeza kuwa suluhisho si kuwadhibiti vijana, bali ni kujenga mifumo yenye uwajibikaji, haki, na kusikiliza kilio cha wananchi, hasa vizazi vipya vinavyotumia teknolojia na mitandao ya kijamii kuhamasisha hoja zao.
Kwa kauli hiyo niliyo quote hapo, inaonyesha Kagame ana hekima kuliko maccm yote kwa pamoja.

Ccm wameshindwa kulitambua hilo wanaishia kuteka, kuumiza, kuua, kufira, kubambikia kesi.

Bila kujua kiini cha tatizo huwezi kulitatua..

By the way, hivi Kagame alimpongeza Bi Chaudele kwa "ushindi wa kimbunga" wa 98% ?
 
Mbona kagame anaongea huku anaingalia tanzania huyu mjuba? Kaitupia jiwe tanzania kimtindo! Yeye mwenyewe tu wananchi wake wana usongo naye, ni dikteta mkomavu. Aombe sana dua gez wake wasisanuke hakuna rangi ataacha kuona
Wanyarwanda hawana usongo na kagame hata kidogo
 
Rais wa Rwanda, Paul Kagame, amesema bara la Afrika linaweza kushuhudia mapinduzi zaidi, hasa kutokana na mtindo wa vijana wa kizazi kipya, maarufu kama Gen Z kuonyesha nia ya kupindua tawala ambazo hazitekelezi matakwa ya wananchi.

Akizungumza kufuatia mfululizo wa mapinduzi barani Afrika, ikiwemo Madagascar mwezi uliopita na machafuko ya kijeshi Guinea-Bissau wiki hii, Kagame amesema ni muhimu viongozi wa Afrika “kujiuliza sababu za mapinduzi haya badala ya kushangazwa nayo.”

Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa, tangu mwaka 1952 kumetokea mapinduzi 130 katika nchi 36 barani Afrika, huku karibu mapinduzi 10 yakitokea ndani ya miaka mitano iliyopita pekee.

Kagame amesema mataifa mengi ya Afrika, ikiwemo Rwanda, yana matatizo katika namna yanavyoendeshwa, jambo linalochochea misuguano kati ya watawala na wananchi. “Namna viongozi wanavyoendesha nchi zao inaweza kujenga mazingira ya mapinduzi,” amesema, akisisitiza kuwa vijana wanafanya hivyo wakiamini wanatafuta mabadiliko ya kiutawala na kiuchumi.

Ameongeza kuwa suluhisho si kuwadhibiti vijana, bali ni kujenga mifumo yenye uwajibikaji, haki, na kusikiliza kilio cha wananchi, hasa vizazi vipya vinavyotumia teknolojia na mitandao ya kijamii kuhamasisha hoja zao.
Chanzo: Mwanahalisi
Huyu naye kwenye democracy ana score chini ya sifuri.
 
Mbona kagame anaongea huku anaingalia tanzania huyu mjuba? Kaitupia jiwe tanzania kimtindo! Yeye mwenyewe tu wananchi wake wana usongo naye, ni dikteta mkomavu. Aombe sana dua gez wake wasisanuke hakuna rangi ataacha kuona
Watu wanasema ana chuki na serikali ya Tz na kundi lililopo sasa madarakani .

Mjuba ni kweli anailenga Tz kimtindo kwenye maneno yake.
 
Back
Top Bottom