Paul Kimiti: Utaratibu wa mtu mmoja kutembea nchi nzima kufuatilia matatizo ya watu hauwezi kufanikiwa

Kazi ya kuutumikia umma upate maendeleo ni networking/kushirikiana na kushirikisha.Siyo kazi ya mjinga mmoja.Haiwezekani.
 
Mheshimiwa Kimiti anasema viongozi wengi hawana misingi ya uongozi na hawana maarifa. [emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Just branding huyo mtu kwenye uso wa shida za watu wasiokuwa na uelewa
 
Heri ya Mmoja asaidiae ,kuliko kukosea kabisa.

Watanzania tuna Imani na MAKONDA C PAUL
 
Wise !!
 
Daah
 
Nadhani hujamuelewa mtoa Mada, yeye ajamlaumu Makonda na utaratibu anao ufanya ila alichosema siyo suruhisho la kutatua matatizo ktk nchi. Kinachotakiwa ni serkali ikishirikiana na chama tawala kujenga misingi imara ya mifumo yote ya utoaji haki.kama ,Mahakam, Polisi, Idara za Ardhi, Tra, halmashauri, Mifumo ya kodi, mifumo ya biashara, kilimo, ufugaji nakadhalika. Ila mtu mmoja kupanda jukwaani nakuanza kuwaita mtendaji mmoja mmoja wa serikali, mfumo huo hauwezi kutatua hata kiduchu matatizo ya wananchi, kwamfano ukienda magerezani kuna maelfu ya watu wanamiaka zaidi ya kumi wapo mahabusu wanasubiri kesi zao zisikilizwe au zinaendelea bila kujulikana zitakwisha lini, wizara ya Ardhi inaongoza kusababisha migogoro ya Ardhi kila kukicha, maafisa TRA wanashutumiwa na wafanya biashara kwa kuwabambikia kesi, Tume ya uchagizi inalaumiwa kwa kuwaweka watu ambao hawakuchaguliwa na wananchi. Hivi ndivyo vitu vinatakiwa kufanyiwa kazi, Makonda ni mtu leo yupo kesho hayupo, ila kukiwa na taasisi imara zinazoweza kujisimamia na kusimamiwa, wala hakuna mtu atakaye kwenda kwa makonda maswala yote yataishia ktk vyombo vinavyohusika.
 
Binafsi nimekuelewa na nimemuelewa mtoa hoja Paul Kimiti pia anachokifanya makonda Kwa nafasi yake kama mwenezi yupo sahahihi tatizo la kinakimiti na watu wengi wanatakiwa kuelewa kwamba hao watatua matatizo ya wananchi wapo huko ila hawawajibiki na wananchi hawatatuliwi shida zao na mishahara wanachukua Kila mwezi Sasa wangekuwa responsible hayo matatizo ya wananchi yasingefika Kwa Makonda .Watumishi wa Umma wamekuwa miungu watu huko walipo na hawamsaidii mh Rais maana amewapa wafanye Kwa niaba yake hawafanyi matokea yake mpaka wananchi walalamike na jambo limfikie yeye kutatua Tena

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Angeulizwa utaratibu upi unaofaha ambao uataza matunda

Makonda amesadia kuonesha uozoo wa serekali hi ya samia
 
Sasa hapo ana msema Nani , aliyemtuma au aliyetumwa.
 
Huyo ni miongoni mwa failed leaders enzi zake nothing was done. Mifumo mmeiua halafu unakuja na hoja mfu. Hii nchi kuna siku wengine mtafukuliwa hata mifupa yenu ishtakiwe
Enzi zao kulikuwa na mifumo thabiti ya kutatua matatizo ya wanaichi.Wakuu wa wilaya na Mikoa walikuwa na muda wa kushughulikia matatizo ya watu.Hivi Sasa muda wa kuwepo ofisini hawana tokana na mfumo ulivyo.Inaonyesha wewe haukuwepo zama hizo ndiyo maana unamtukana Mzee huyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ