Nadhani hujamuelewa mtoa Mada, yeye ajamlaumu Makonda na utaratibu anao ufanya ila alichosema siyo suruhisho la kutatua matatizo ktk nchi. Kinachotakiwa ni serkali ikishirikiana na chama tawala kujenga misingi imara ya mifumo yote ya utoaji haki.kama ,Mahakam, Polisi, Idara za Ardhi, Tra, halmashauri, Mifumo ya kodi, mifumo ya biashara, kilimo, ufugaji nakadhalika. Ila mtu mmoja kupanda jukwaani nakuanza kuwaita mtendaji mmoja mmoja wa serikali, mfumo huo hauwezi kutatua hata kiduchu matatizo ya wananchi, kwamfano ukienda magerezani kuna maelfu ya watu wanamiaka zaidi ya kumi wapo mahabusu wanasubiri kesi zao zisikilizwe au zinaendelea bila kujulikana zitakwisha lini, wizara ya Ardhi inaongoza kusababisha migogoro ya Ardhi kila kukicha, maafisa TRA wanashutumiwa na wafanya biashara kwa kuwabambikia kesi, Tume ya uchagizi inalaumiwa kwa kuwaweka watu ambao hawakuchaguliwa na wananchi. Hivi ndivyo vitu vinatakiwa kufanyiwa kazi, Makonda ni mtu leo yupo kesho hayupo, ila kukiwa na taasisi imara zinazoweza kujisimamia na kusimamiwa, wala hakuna mtu atakaye kwenda kwa makonda maswala yote yataishia ktk vyombo vinavyohusika.