samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Naomba kutoa dukuduku langu kuhusu huyu mtangazaji wa star tv ambaye mara kadhaa hutangaza kipindi cha tuongee asubuhi kinachorushwa na star tv kila siku kuanzia sa moja na nusu asubuhi hadi sa tatu kamili. Binafsi mtangazaji huyu nimekuwa sipindezwi naye kwa namna anavyoendesha kipindi cha tuongee asubuhi. Nina sababu kuu tatu zinazonifanya nisipendezwe na namna jamaa huyu anvyoendesha kipindi hicho. Mosi, paul mabuga amekuwa na tabia ya kuegemea upande moja hasa ule unaotetea serikali kitu ambacho hatakiwi kukionesha waziwazi yeye akiwa kama mtangazaji.(hapa nazungumzia mada zinazohusisha ukosoaji wa serikali). Katika hili paul mabuga amejipambanua waziwazi kwamba yeye ni kada wa chama cha kijani. Yeye kama mtangazaji anapaswa kusimama katikati pasi kuegemea upande wowote. Pili, paul mabuga amekuwa na tabia ya kuwakatisha wazungumzaji walioalikwa studio mara kwa mara kwa kupachika vijimaswali vya ajabu ajabu kabla hawajamaliza kuzungumza kile walichokuwa wanakieleza. Kwa sababu hiyo amekuwa akipoteza mwelekeo wao wa kuchangia hasa pale wanapokua wanaibana serikali. Nambuka wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana mabuga alimualika dr slaa studio kwenye kipindi hicho ambapo hakutaka kumpa nafasi dr slaa kuzungumza kwa kina na mara nyingi alikua akimkatisha mara kwa mara na kumuuliza vijimaswali visivyo na tija, nakumbuka ilifika wakati dr slaa aliishiwa uvumilivu akamwambi kama hutaki nijieleze ni bora usingenialika hapa studio.. Sababu ya tatu ni kutokana na tabia yake ya kubana muda wa kupiga simu kwa wachangiaji wanaofuatilia kipindi hicho. Mara nyingi anapoendesha kipindi utakuta anaruhusu simu zikiwa zimesalia dakika 20 au 15 kabla ya kipindi kumalizika natokeo yake wanapiga simu watu wawili au watatu kipindi kinamalizika. Hii inaondoa zana ya tuongee asubuhi. Namshauri paul mabuga aige mfano wa watangazaji wenzake samadu hassan na rymond nyamwihula ambao wamekua wakiendesha kipindi hicho kwa uhodari mkubwa na kuwapa waalikwa uhuru wa kuzungumza bila kukatishwa mara kwa mara Nawasilisha.. .