Nachoamini ni kuwa changamoto ni jambo la kawaida kwa binadamu! Kwangu mimi hakuna hoja ya kipuuzi. Lakini pia binadamu kutofautiana katika fikra ni jambo la kawaida, fikra zinajengwa na misingi minigi, baadhi ni pamoja na Imani, utashi na uelewa. Siwezi kuhukumu kipi kinawasukuma baadhi kutoa hoja na maoni waliyonayo, lakini ni mara chache misingi hii ikafanya katika hali ya usawa na kwa pamoja,lazima msingi mmoja utakuwa juu zaidi ya mingine. Kama binadamu pia kuna hatua za kujifunza katika jambo, kwanza naona, Napata uzoefu, maarifa mapya kama yapo na kisha napambanua, na hii ni lazima.
Kuibuka na fikra na kushtumu ama kulalamikia jambo ambalo una uewlewa nalo ama huna pia siyo dhambi, lakini uendeshaji na utayarishaji wa vipindi vya majadiliano una misingi na maadili yake. Unaweza kufanya kama wengine wanavyotaka uwafurahishe, nap engine fikiria ukifanya kuegemea upande mwingie kuwauzi hali itakuwaje. Lakini fikiria ukaendesha mjadala ambao wageni wako wengi wa upande mmoja, lakini unatakiwa kuwa na muungwana akilalamika kwa sababu umeuliza jambo ambalo yeye linamkirihisha.
Najua kwa nini zinakuwepo hoja kama zinazotolewa, lakini naziheshimu na nachukua kama changamoto.
Pengine ni nadra kwa mtu kujibu wazi malalamiko kama hivi, lakini nawapeni hongera mnaotoa malalamiko, wengine nawafahamu na wengine siwajui lakini Shukurani na Kwaresma njema.