Paul Mackenzie apatikana na hatia kwa Mauaji 191 ya Shakahola, hukumu kutolewa Novemba 6

Paul Mackenzie apatikana na hatia kwa Mauaji 191 ya Shakahola, hukumu kutolewa Novemba 6

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
1792428790508.png

Mahakama Kuu ya Mombasa imempata mhubiri Paul Nthenge Mackenzie na hatia kwa mashtaka yote 191 ya mauaji yanayohusiana na janga la Shakahola, katika kesi iliyotikisa Kenya kufuatia kugunduliwa kwa mamia ya miili katika msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi.

Jaji Diana Kavedza-Mochache ametoa wamuzi huo leo Jumatatu, Oktoba 19, 2026, baada ya kusikiliza kesi iliyohusisha Mackenzie na washtakiwa wenzake kuhusu vifo vya watu 191, wakiwemo watoto 190 na mtu mzima mmoja.

Hata hivyo, adhabu ya Mackenzie bado haijatolewa. Mahakama imepanga kutoa hukumu ya adhabu Novemba 6, 2026.

Kesi hiyo ilihusu vifo vilivyohusishwa na shughuli za kanisa la Good News International, lililokuwa likiongozwa na Mackenzie.

Upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi uliolenga kuthibitisha kuwa wafuasi walishawishiwa kufunga kula kwa imani kwamba wangekutana na Yesu. Ushahidi pia uliangazia mazingira ambayo watoto walipoteza maisha.

Katika janga hilo pana la Shakahola, mamia ya miili ilifukuliwa kutoka katika makaburi ya halaiki, na tukio hilo likazua maswali kuhusu ulinzi wa watoto, udhibiti wa taasisi za kidini na hatua zilizochukuliwa na mamlaka kabla ya vifo hivyo kugunduliwa.

Macho yote sasa yanaelekezwa Novemba 6!

Wamuzi wa kumtia Mackenzie hatiani ni hatua muhimu katika kesi hiyo, lakini tarehe ya Novemba 6 ndiyo itakayofafanua adhabu atakayopokea. Kesi hiyo imeendeleza mjadala kuhusu uwajibikaji wa viongozi wa kidini na wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa uhuru wa kuabudu hauwi kisingizio cha kuhatarisha maisha ya Wananchi.

Baada ya Mackenzie kupatikana na hatia kwa mashtaka yote 191, ni hatua gani Kenya inapaswa kuchukua ili kuimarisha usimamizi wa taasisi za kidini na kuzuia janga kama la Shakahola lisijirudie?
 
Huyu mchungaji anatakiwa ale chuma live au kunyogwa siku moja baada ya hukumu yaani november 7 saa sita mchana kwenye viwanja vya moi kasalani mbela ya halaiki
 
Back
Top Bottom