Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Wakili wa mjibu maombi Paul Makonda, ameieleza Mahakama ya wilaya ya Kinondoni kuwa mteja wake bado hajapokea hati yoyote ya wito wa Mahakama dhidi yake, zaidi ya kuzipata taarifa hizo kupitia vyombo vya habari.
Wakili huyo aliyejitambulisha kama Goodchance Regnald ameyasema hayo leo mbele ya Hakimu Aron Ryamuya katika kesi ya maombi ya kufunguliwa kwa kesi ya jinai dhidi ya Paul Makonda, DPP na DCI katika mahakama hiyo.
Wakili Goodchance ameongeza kwa kusema kuwa Makonda hakupata hati rasmi ya wito zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari, na hivyo akaamua kumtuma wakili wake kuja mahakamani.
Baada ya Wakili Goodchance kueleza hayo akaiomba Mahakama kumpa hati hiyo ya wito ambayo mteja wake ataijibu, jambo ambalo Hakimu Ryamuya aliamuru kufanyika leo.
Source Makonda amtuma wakili wake mahakamani