Pre GE2025 Paul Makonda ameagiza Waziri wa TAMISEMI kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Pangani Haraka Sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwani si wangepigiana simu na Waziri, kuna sababu gani ya kupayuka majukwaani ili tuone kuwa wanafanya kazi wakati CCM = Serikali tu....
Lazima chama kiwape taarifa wananchi juu ya hatua mbalimbali zinazokuwa zinachukuliwa na chama chao na serikali yao juu ya kero zao . Chama hakiwezi kukaa kimya halafu wananchi waendelee kunung'unika tu bila kujuwa hatua zinazofanywa na serikali yao.

Wananchi wana haki ya kupewa taarifa na siyo kufanya mambo kimya kimya tu.

Hii ndio maana ya CCM kuwa chama kiongozi hapa nchini na barani Afrika
 
wazembe na wafanyakazi kwa mizaha na mazoea wawajibishwe vizuri sana na kwa haraka sana pia..
 
Hahaha we all knows inaishia kwenye maneno na hana mamlaka kisheria kuagiza watumishi wa serikali, na hakuna litalo fanyika
Sasa wewe jidanganye ufanye uzembe halafu ukutwe na kubainika .kwa hakika utakiona cha mtema kuni na kujuta kuzaliwa.
 
Chama kushika hatamu kumbe bado kupo katika kipindi hiki cha vyama vingi?
CCM Ndio yenye serikali na katika hilo haipaswi kufumbia macho na kuwaonea hata watendaji na watu wanaofanya kazi kwa mazoea na kuwaacha wananchi wakiteseka kupata haki na huduma kwa wakati. Sasa wewe mtu amefanya kazi amekupa bidhaa au vifaa vya ujenzi kwa mkataba wa malipo ya muda fulani. Halafu muda unafika unaanza kuleta kiburi katika ulipaji bila kujali wengine wamekopa pesa benki zinazohitajika kufanya marejesho bila kuchelewa .sasa unataka watoe wapi pesa za marejesho?
 
Mbaya sana nchi kuendeshwa Kwa matakwa ya chama. Maeneo ambapo mtu asokuwa wakijani ni kiongozi ataundiwa zengwe alimradi wanakijani ndiyo waongoze kila idara na ukiwa kijani kiherehere hata ukikosea utalindwa
 
Sasa wewe kaa usifanye kazi au ufanye kazi kwa mazoea halafu uanze kusema mbuzi wa kafara.
Kazi lazima nifanye, Ila sio unavyotaka wewe.

Ila wafanya Kazi Kwa mazoea mnao huko huko juu na hamuwagusi.

Vidagaa chini ndio vinatolewa mbuzi wa Kafara.

Hivyo Acha unafiki.
 
Kazi lazima nifanye, Ila sio unavyotaka wewe.

Ila wafanya Kazi Kwa mazoea mnao huko huko juu na hamuwagusi.

Vidagaa chini ndio vinatolewa mbuzi wa Kafara.

Hivyo Acha unafiki.
Hakuna mvivu na mzembe kazini atakaye bakia salama wakati huu. Maana chama hakipo tayari kuchonganishwa na wananchi kwasababu ya uzembe wa watu wachache walioamua kufanya kazi kwa mazoea na kushindwa kubadilika.
 
Mbaya sana nchi kuendeshwa Kwa matakwa ya chama. Maeneo ambapo mtu asokuwa wakijani ni kiongozi ataundiwa zengwe alimradi wanakijani ndiyo waongoze kila idara na ukiwa kijani kiherehere hata ukikosea utalindwa
Haangaliwi mtu sura yake katika kumuwajibisha. Kinachoangaliwa ni utimizwaji wa majukumu na kuwajibika.ukishindwa kutimiza majukumu yako ni lazima uwajibishwe Bila kuangalia wewe ni nani.
 
Haangaliwi mtu sura yake katika,aje kilimo maana viwanda vyasukari vinakosa miwa kumuwajibisha. Kinachoangaliwa ni utimizwaji wa majukumu na kuwajibika.ukishindwa kutimiza majukumu yako ni lazima uwajibishwe Bila kuangalia wewe ni nani.
Mwambieni aanzie juu kwanini anakimbilia chini,umeme nijambo hovyo kabisa nchi hii...aanzie na waziri wa nishati kisha aje kilimo maana hatuna sukari,mafuta nk. Pia aende mifugo nk. nk.
 
Mwambieni aanzie juu kwanini anakimbilia chini,umeme nijambo hovyo kabisa nchi hii...aanzie na waziri wa nishati kisha aje kilimo maana hatuna sukari,mafuta nk. Pia aende mifugo nk. nk.
Hakuna jiwe litakalobakia pasipo kugeuzwa ikibainika ni kikwazo katika safari ya kuelekea nchi ya kanaan
 
Elewa na kufahamu ya kuwa Mheshimiwa Paul Makonda ndiye msemaji wa CCM. Kwa hiyo akisema Makonda ni chama kinakuwa kimesema kupitia ulimi wa msemaji wake Taifa.
 
Huyu Mtu Uthubutu wake ni zaidi ya JPM.


Watu aina ya Makonda ni muhim sana kwenye kufanikiwa
Nilishasema Makonda ni kijana jasiri sana kwa wakati huu katika ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara. Ni nadra sana kupata viongozi majasiri na wasio ogopa kitu kama alivyo paul Makonda. Makonda ni hazina kwa Taifa letu.
 
Mimi nimeandika sentensi moja, kwanini unijazie page nzima afu pumba?! Siku ingine don't respond to my post. Sawa?!
 
Tayari amesha simamishwa kazi Mkurugenzi wa Pangani kama ambavyo Mheshimiwa Makonda ametoa maagizo ya chama kwa waziri wa TAMISEMI juu ya kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo.kutokana na malalamiko.mengi aliyokutana nayo katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.
 
Mbona yeye anazuia uwajibikaji?

Kwanini mlizuia asikaguliwe jambazi aliyekua anachipukia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…