Paul Makonda ni kiungo wa kuaminiwa anaupiga namba yoyote atakayopangiwa

Paul Makonda ni kiungo wa kuaminiwa anaupiga namba yoyote atakayopangiwa

Joined
Nov 6, 2016
Posts
77
Reaction score
271
USHUPAVU WA PAUL MAKONDA UNAMFANYA KUWA KIUNGO MUHIMU KATIKA CHAMA, KOCHA ANAMCHEZESHA POPOTE

Na Comrade Ally Maftah

Mimi ni shabiki mkubwa wa aina za siasa anazofanya Paul Makonda, naweza kusema ndio mwanasiasa kinara kati ya miongo miwili yenye mabadiliko makubwa ya mitindo ya siasa, ukuaji wa uchumi na maendeleo ya teknolojia.

Uwezo wa makonda kwenye kupangilia mambo yaendane na mandhari ya siasa inamfanya kuendelea kuwa kiongozi na mwanasiasa bora kuwahi kutokea.

Kuna minongono mingi kuhusu Paul Makonda kupelekwa Arusha ila mimi nasema Jemedali yupo kazini na Dr Samia yupo imara sana kupanga safu yake kuingia kwenye chaguzi mbili zilizopo mbele yetu, uchàguzi wa serikali za mitaa 2024, na uchaguzi mkuu 2025.

SISI WANA CCM VINDAKINDAKI TUNAUONA USHINDI WA HESHIMA KWA DR SAMIA UKIOGELEA KWENYE CHAMA CHETU CHENYE HAZINA KUBWA YA VIONGOZI WENYE VIPAJI LUKUKI,

TUNA IMANI NA DR SAMIA
PAUL MAKONDA JEMEDARI PIGA KAZI TENA.

Ndimi Comrade Ally Maftah
Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam
IMG-20240330-WA0082.jpg
 
Kiraka,, watu wanajua kashushwa,,,,,kazi ya jeshi kambi popote
 
Ali ali nakuita mara ya tatu ali. Kiongozi wa serikali yoyote anaweza teuliwa popote na akafanya kazi. Pia hata wewe.

Acha ujinga wa kusifia. Or else usijiite comrade.

Tutakutoa macomrade wenzako wakiume sisi.
 
Ajifunzetu kuwa na akiba ya maneno. Umri wake bado mdogo kwenye maisha ya siasa
 
Ivumayo Haidumu
Mwamba Ngoma Huvutia Kwake
 
Ule mkwara kwa GSM sasa kwisha ngoja aje huku Chuga tukimbizane kwenye Migomba.
 
Makonda ana damu nyingi za watu. Hata Wamerekani wanajua. Samia aliwachanganya watu kupitisha zigo lake la DP WORLD ndio akamteua makonda ili tension iwe kwa Makonda.
 
Unaweza ukamchukia Makonda lakini lijapo suala la ushawishi huyo binadamu anao ushawishi wenye wingi was kipimo.

Tunaweza kumdhihaki Paul na kumbeza, lakini, Musukuma yule kaaga na kuagwa kwao kwa agano la simiko la KUTISHA!
 
Back
Top Bottom