Paul Makonda: Ukitaka kujua kwanini Tanzania ni maskini pitia mkataba wa Yanga wanaosaini Leo

jang

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
1,415
Reaction score
1,186
Alianza Zito, akaja tundu lisu, sasa makonda. Huo mkataba una nini?? Tunaomba uwekwe wazi kwanza kabla ya kupitishwa


====================
Makonda atoa ya moyoni kuhusu Yanga, aihusisha Yanga na umasikini kwa watanzania

Kitendo cha klabu ya Yanga kumruhusu mwnyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji kuikodi klabu hiyo kwa miaka 10 kinaonekana kuendelea kuwagusa watu wengi na mmoja wapo amekuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye pamoja na kuguswa na kitendo hicho pia ameamua kuandika katika mitandao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda aliandika “Unataka kujuwa kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na UTAJIRI MKUBWA WA MALIASILI tulizonazo? Soma Mkataba wa Yanga wanaosaini LEO”

Baada ya kuweka picha hiyo wadau mbalimbali wa soka nchini wamekuwawakiweka maoni yao katika picha hiyo, wengine wakimtaka asizungumze mambo ya Yanga, wengine wakimtaka afanye kazi za serikali na aache kujihusisha na soka na mashabiki wa wapinzani wa Yanga wakiwasema watani wao wa jadi kwa kukubali timu yao kukodishwa kwa mtu mmoja na akiwaachia majengo.

Awali Makonda aliweka picha ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na kusema kuwa alikuwa na maswali 87 kwa kiongozi huyo wa Yanga lakini baada ya kutizama mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha Clouds Tv aligundua kwamba kiongozi huyo bado hajaelewa ni kitu gani kinaendelea klabuni.
 
makonda anaelewa kuwa masuala ya michezo hayaingiliwi na serikali?....kwahiyo ajitahidi kuongea kama mshabiki au mwanachama wa yanga na sio kiongozi wa serikali. na afuate taratibu na kanuni za uendeshaji wa vilabu vya mipira tanzania na duniani....vikao ndiko hutolewa maoni na malalamiko...sasa anapokuja kutoa kwenye mitandao ya kijamii kwanini hakuuliza kwenye mkutano mkuu wa jumamosi iliyopita?
 
Makonda ni shabiki wa mkia
 
Akiingiza unazi wake kwenye timu hizi mbili atashangaa kapelekwa Mkoa mpya wa Mbekenyela.
Kapuya yuko wapi?
 
Unataka kujuwa kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na UTAJIRI MKUBWA WA MALIASILI tulizonazo?

Soma Mkataba wa Yanga wanaosaini LEO.


Source : Facebook page
 
Sasa anaongea nini baada aongelee mikataba ya selikari anaongelea mambo ya yanga

Ya yanga yanamalizwa na wanachama wa yanga

Sisi tunataka kusikia uuzwaji wa coco beach , Uda, Machinga complex ,,,,
e t c
 
Kabla ya kurukia mikataba ya wana yanga tupitie kwanza mikataba 17 ya wachina walio ingia na serikali
 
Unataka kujuwa kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na UTAJIRI MKUBWA WA MALIASILI tulizonazo?

Soma Mkataba wa Yanga wanaosaini LEO.


Source : Facebook page

Afadhali mkataba wa Yanga tutauona mikataba ya gesi mbona hatuioni.
 
Sasa anaongea nini baada aongelee mikataba ya selikari anaongelea mambo ya yanga

Ya yanga yanamalizwa na wanachama wa yanga

Sisi tunataka kusikia uuzwaji wa coco beach , Uda, Machinga complex ,,,,
e t c
Mi nilifikiri huyu jamaa angetuambia kwamba tunataka kujua kwa nini Dar ni chafu hadi leo tunakumbwa na kipindupindu, basi tusome mikataba ya usafi baina ya kampuni za kuzoa taka na halmashauri za jiji...........
 
Mi nilifikiri huyu jamaa angetuambia kwamba tunataka kujua kwa nini Dar ni chafu hadi leo tunakumbwa na kipindupindu, basi tusome mikataba ya usafi baina ya kampuni za kuzoa taka na halmashauri za jiji...........
Mkuu tatzo ni mpuuzi tu na tunatakiwa kupuuza story zake za kijinga!!
 
Huyu dogo ana matatizo! Mi staki hata kusikia maneno yake! Ni kama boss wake! Anachokiwaza anakiongea bila kutafakari.

Eti aondoe ombaomba Dar
Eli walimu wasilipe nauli

eti .... yaani mambo ya ajabu ajabu
 
Huo mkataba kauona wapi?
Je ule we Mo kuinunua Simba kauona au bado?
 
Afadhali mkataba wa Yanga tutauona mikataba ya gesi mbona hatuioni.
Ile mikataba ya kichina inatutia mashaka sana maana inawezekana tukawa tumepigwa bei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…