Paul Makonda: Ukitaka kujua kwanini Tanzania ni maskini pitia mkataba wa Yanga wanaosaini Leo

Paul Makonda: Ukitaka kujua kwanini Tanzania ni maskini pitia mkataba wa Yanga wanaosaini Leo

Haw

Hawa jamaa wamebanwa kodi kwenye biashara zao sasa kwa kuwa kwenye vilabu hivo masuala ya kodi ni kama sifuri hivo wanafanya kila wawezavo kujikita huko. Naomba serikali itupie jicho huko kama ilivofanya kwenye taasisi za kidini. Kama kweli wanapesa na ni wapenzi wa soka waanzishe vilabu vyao kama Azam FC.

Acha mawazo ya kipumbavu kwani lazima waanzishe hata kununua au kukodisha poa ilimradi watu wamekubaliana
 
Mimi najuwa kinachokodishwa ni MAJAMVI....SUFURIA....nk lakini timu haikodishwi.
 
Alianza Zito, akaja tundu lisu, sasa makonda. Huo mkataba una nini?? Tunaomba uwekwe wazi kwanza kabla ya kupitishwa


====================
Makonda atoa ya moyoni kuhusu Yanga, aihusisha Yanga na umasikini kwa watanzania

Kitendo cha klabu ya Yanga kumruhusu mwnyekiti wa klabu hiyo, Yusuph Manji kuikodi klabu hiyo kwa miaka 10 kinaonekana kuendelea kuwagusa watu wengi na mmoja wapo amekuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye pamoja na kuguswa na kitendo hicho pia ameamua kuandika katika mitandao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda aliandika “Unataka kujuwa kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na UTAJIRI MKUBWA WA MALIASILI tulizonazo? Soma Mkataba wa Yanga wanaosaini LEO”

Baada ya kuweka picha hiyo wadau mbalimbali wa soka nchini wamekuwawakiweka maoni yao katika picha hiyo, wengine wakimtaka asizungumze mambo ya Yanga, wengine wakimtaka afanye kazi za serikali na aache kujihusisha na soka na mashabiki wa wapinzani wa Yanga wakiwasema watani wao wa jadi kwa kukubali timu yao kukodishwa kwa mtu mmoja na akiwaachia majengo.

Awali Makonda aliweka picha ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na kusema kuwa alikuwa na maswali 87 kwa kiongozi huyo wa Yanga lakini baada ya kutizama mahojiano aliyofanyiwa na kituo cha Clouds Tv aligundua kwamba kiongozi huyo bado hajaelewa ni kitu gani kinaendelea klabuni.
Huyu nae punga kweli,,mikataba ya gesi mbona wanaficha
 
Muambieni "the boss is back"
Pyepyeewww..!! Maandamano fc wajipange haswa ,la sivyo ubingwa utakuwa rufaa ya pili FIFA.
 
Nilishangaa jana mmoja wa maaskofu waliokuwepo uwanja wa Karume katika sala zake kwa mungu wake, jina makonda Paul liliombewa.

Maana yake nini?
 
Back
Top Bottom