Pauline Gekul: Ari, Bidii na Uzalendo imetuletea Ushindi Dhidi ya Ufaransa

Pauline Gekul: Ari, Bidii na Uzalendo imetuletea Ushindi Dhidi ya Ufaransa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Ari, Bidii na Uzalendo imetuletea Ushindi Dhidi ya Ufaransa : Mhe. Gekul

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul ameipongeza timu ya Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls) kwa ushindi wa magoli mawili kwa Moja dhidi ya Ufaransa.

Mechi hiyo ya Kundi D iliyochezwa Oktoba 15, 2022 Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru Jijini Goa, nchini India imeipandisha Tanzania hadi nafasi ya pili nyuma ya Japan na mbele ya Canada na Ufaransa katika kundi hilo.

"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan inatoa mchango mkubwa kwa timu zinazowakilisha nchi vyema, na ndio maana hata nyie Serengeti Girls Serikali ipo hapa na nyie kuhakikisha inawaunga mkono ili mfanye vizuri" amesema Mhe. Gekul

Kwa upande wake Kocha wa timu Bakari Shime, amesema vijana wanaendelea kuimarika na kusahihisha makosa ya mechi ya kwanza na Japan ambayo leo umeleta matokeo mazuri.

" Kesho tutaelekea Mumbai na tukifika tutafanya mazoezi kwa ajili ya mchezo na Canada ambao tukishinda tunasonga mbele," amesema Kocha Shime.

Tanzania ipo katika kundi D pamoja na Japan, Ufaransa na Canada.

IMG-20221016-WA0007(1).jpg

IMG-20221016-WA0008(2).jpg

IMG-20221016-WA0008(2).jpg

IMG-20221016-WA0009(2).jpg

IMG-20221016-WA0010(2).jpg

IMG-20221016-WA0011(2).jpg
 
Back
Top Bottom