Huyu dogo kailetea Juve balaa huko Serie a,penati yake ya dk ya 97 juzi iliiua Milan 2-1,Donnaruma aliwasumbua sana maforward wa Juve throughout tthe match anadaka hadi milingoti kuhakikisha Juve hawashindi ile mechi.
Kuona vile wakamuundia zenngwe,Higuain kalenga shuti mkononi mwa beki,penati wakapata Juve,mjomba Dybala akamwambia Donnaruma hapa bwamdogo nakutia adabu siku nyingiine usijifanye wewe ni Buffon,na nakupelekea huko huko kulia unakoruka tuone kama utaidaka!Donnaruma kajinyoosha hadi kucha lakini wapi,.nyavu ndogo zinatikisika na mpira umeisha!akapigapiga nyasi za Juventus stadium hakuridhika,akataka kumtwanga refa,kocha wake Montela akamzuia,hasira zake akawaambia wachezaji wenzie kule locker room wakachanachana banners zote za Milan zilizobandikwa ukutani,wakaona haitoshi wakang'oa na viti vya locker room,Hivi Juve hawajamaliza kutengeneza viti vyao leo zamu ya Casillas nae kanyooshwa na Dybala huyu huyu!sijui viti vimesalimika huko.Waache kumpa penati huyu dogo anautia hasara uwanja wa Juve!