Tuko katika wakati mgumu sana! ingawa tuna kabiliwa na matatizo mengi yanayo pelekea hata Maaskofu, Masheghe, Mapadri na watu tofauti ambao hapo awali hawakuonekana katu kujihusisha na Siasa hata kidodo lkn sasa wameshindwa kuvumilia na kuamka katika nafasi zao kuingilia yanayo tupata, na hali hii imepelekea hata jamii kuona kwamba kuna namana fulani ambapo siasa inatutenganisha, kwa mtazamo wangu palipo na mkusanyiko ya waelewa kama hapa JF ambao karibia wote tuna nuia mamoja na kujadili yanayo husu jamii yetu na maisha kwaujumla basi pengine ipo haja ya walau kutiana na kushirikishana katika imani zetu na sio kutofautiana, hii yote ikilenga kurudisha ule unaosadikiwa kuwa ni ufa kati ya waumini wa dini zetu tunazo abudia, Tuna oana, tunashirikishana, tunazikana, tunasaidiana, Mimi ni Mkristo Akiniambia imani Muislamu kwanini Dini yake inasemaje juu ya Ufisadi, kesho nitamwambia mimi Juu ya Ubakaji, tofauti hakika najua lazima zitakuwepo lkn nia ikiwa kuelimishana na si kukosoana basi huyu atajifunza kwa yule na yule atajifunza kwa huyu. Pasiwepo nafasi ya kujadili tofauti rather iwepo nafasi ya kujadili Yanayo wiana tukiweka msisitizo kujengana ki imani.