Pawepo na page inayo jadili mambo ya kiroho

Pawepo na page inayo jadili mambo ya kiroho

B4U

Member
Joined
Dec 31, 2010
Posts
24
Reaction score
0
Tuko katika wakati mgumu sana! ingawa tuna kabiliwa na matatizo mengi yanayo pelekea hata Maaskofu, Masheghe, Mapadri na watu tofauti ambao hapo awali hawakuonekana katu kujihusisha na Siasa hata kidodo lkn sasa wameshindwa kuvumilia na kuamka katika nafasi zao kuingilia yanayo tupata, na hali hii imepelekea hata jamii kuona kwamba kuna namana fulani ambapo siasa inatutenganisha, kwa mtazamo wangu palipo na mkusanyiko ya waelewa kama hapa JF ambao karibia wote tuna nuia mamoja na kujadili yanayo husu jamii yetu na maisha kwaujumla basi pengine ipo haja ya walau kutiana na kushirikishana katika imani zetu na sio kutofautiana, hii yote ikilenga kurudisha ule unaosadikiwa kuwa ni ufa kati ya waumini wa dini zetu tunazo abudia, Tuna oana, tunashirikishana, tunazikana, tunasaidiana, Mimi ni Mkristo Akiniambia imani Muislamu kwanini Dini yake inasemaje juu ya Ufisadi, kesho nitamwambia mimi Juu ya Ubakaji, tofauti hakika najua lazima zitakuwepo lkn nia ikiwa kuelimishana na si kukosoana basi huyu atajifunza kwa yule na yule atajifunza kwa huyu. Pasiwepo nafasi ya kujadili tofauti rather iwepo nafasi ya kujadili Yanayo wiana tukiweka msisitizo kujengana ki imani.
 
basi pengine ipo haja ya walau kutiana na kushirikishana katika imani zetu na sio kutofautiana.

Hapo kwenye red naunga mkono asilimia 101% na naunga mkono hoja
 
Ni dhahiri shahiri wakati huu ni muafaka kwa kuwa na ulingo huo wa IMANI, ITATUSAIDIA SANA KUELIMISHANA na pia kasoro kadha wa kadha kuepukika kwa muelimisho mwema.
 
Naunga mkono hoja tena kwa ukamilifu.
 
Hivi ile forum ya DINI ambayo ipo inatofauti gani na unachokiomba??
 
1.mijadala ya dini za kiislamu,huwa haipo katika mambo wanayokubaliana bali wanayotofautiana.
Mfano.
1.yesu si mungu.
2.muhamad si nabii
3. Kiti moto ni halali.
Hizo ndizo mada zinazotawala.
Siungi mkono hoja hiyo.
 
Mimi naomba tu kutoa ushauri, unapolog in JF jipe walau dakika tano usifunguwe thread yoyote na wala usichangie thread yoyote, wewe ikaguwe vizuri tu utakuta vitu vingi mnavyouliza vipo humu ila shida mtu akishalog in tu basi anarukia kwenye mada, ndio maana utakuta thread nyingi zinajirudia, lakini tusingekuwa na pupa tungekuwa tunaona kila kila kitu. mkuu jukwaa la dini lipo humu, nenda uko utakutana na masharti yake ya kujiunga na hilo jukwaa. na hapa ninapocomment hii thread yako ni watu wawili tu ndio tunaview hii topic yako sasa hivi. maana wazoefu humu huwa hawana muda wa kupoteza.
 
Mimi naomba tu kutoa ushauri, unapolog in JF jipe walau dakika tano usifunguwe thread yoyote na wala usichangie thread yoyote, wewe ikaguwe vizuri tu utakuta vitu vingi mnavyouliza vipo humu ila shida mtu akishalog in tu basi anarukia kwenye mada, ndio maana utakuta thread nyingi zinajirudia, lakini tusingekuwa na pupa tungekuwa tunaona kila kila kitu. mkuu jukwaa la dini lipo humu,


kama ungesoma vizuri maoni yake bila kukimbilia kujibu ungeelewa huyu bwana/bibi hoja yake inasimama yenyewe bila uhusiano na jukwaa la dini, au ili kwa hoja yako kuwa na mashiko inabidi jukwaa la dini nalo lifanyiwe mabadiliko.
 
kama ungesoma vizuri maoni yake bila kukimbilia kujibu ungeelewa huyu bwana/bibi hoja yake inasimama yenyewe bila uhusiano na jukwaa la dini, au ili kwa hoja yako kuwa na mashiko inabidi jukwaa la dini nalo lifanyiwe mabadiliko.


Mambo ya kaizari mpe kaizari, mambo ya dini yakajadiliwe kwenye jukwaa la dini. PERIOD.
 
Hivi ile forum ya DINI ambayo ipo inatofauti gani na unachokiomba??

Hata mimi ndo nataka nijue kama kuna tofauti yeyote???!!! Pengine hajaiona! Ana post 4 tu tangu aanze kazi hapa JF, ingawaje kajiunga kabla yangu. Sina uhakika kama kaiona forum ya dini au la, tumuulize
 
umerudishiwa nguvu zako za kuweka avatar?naona souljah anakula moja moja

Mkuu kama unavyoona ktk Avatar mpya, sitaki masihara saa hizi! Nakanyaga hadi Invisiboooooooooooooooo! Hahahahahah!
 
Hii hoja ina utata kidogo, je hilo jukwaa lijadili mambo ya kiroho to what extent!!!! Kuna mambo mengi hayajadiliki kama hizo hoja alizozitoa Tall.. Ni vigumu sana kujadili mambo ya kiroho bila kuhusisha dini, na hizi dini zote zimejengwa kwa misingi yake ambayo kamwe haitobadilika na kuanza kuijadili hapa ni kuleta vurugu tu.. Ukimwambia muislam Muhamad S.A.W sio mtume wakati uislam umejengwa katika mafundisho yake na imani kuwa ni mtume kama watakubali maana yake uislam haupo. Vivyo hivyo kwa wakristu sababu ya kristo ambaye kwao ni Mungu. Bado wahindu nao waje na Miungu wao, hapo bado ambao ukoloni haukupita kwao waje na mizimu yao....... hakutokuwa na amani katika jukwaa hilo... Nawasilisha hoja!:kev:
 
Sina hakika kama nimekuelewa vizuri but unaweza kuwapm mods wakuruusu uingie kwa wakubwa ndo utaona kuwa tayari jukwaa hilo lipo ingawa wakati mwingine tunalimiss use cheki hapa
Dini/Imani
Karibu, hapa si mahala pa mihadhara bali masuala kuhamasishana kiimani na kufundishana yale yaliyo mema. Aidha ni sehemu muafaka kuangalia mapungufu katika dini zetu na kuuliza maswali kwa waamini wa dini husika kuhusu imani yao. Contact Invisible to get access!
 
Majadiliano ya dini tangu niyajue sijawahi kuona yakiisha hata siku moja.
 
Back
Top Bottom