Uchaguzi 2020 Pazia la kutangaza nia lafunguliwa ACT - Wazalendo

Uchaguzi 2020 Pazia la kutangaza nia lafunguliwa ACT - Wazalendo

Ado Shaibu

Member
Joined
Jul 3, 2010
Posts
99
Reaction score
111
TAARIFA KWA WANACHAMA NA WAPENZI WA ACT WAZALENDO.

Kama inavyofahamika, 2020 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Kwa upande wa Zanzibar, watachagua pia Rais wa Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Chama cha ACT Wazalendo kimejipanga kushiriki na kushinda kwenye chaguzi za Urais, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani.

Katika kipindi hiki ambapo wanachama wanasubiri ratiba ya uchukuaji fomu na vikao vya uteuzi wa wagombea, tunapenda kuwakumbusha wanachama wa ACT Wazalendo kuwa kanuni na taratibu za ACT Wazalendo zinaruhusu wanachama kutangaza nia ya kugombea nafasi wanazozitaka kwenye uchaguzi.

Ofisi ya Katibu Mkuu inawakumbusha kuwa;

1. Kila mwanachama ana uhuru wa kujitangaza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu nia yake ya kugombea nafasi yoyote anayotaka kugombea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

2. Makatibu wa Kata na Majimbo wameagizwa kuandaa madaftari ya watia nia katika maeneo yao ambayo kila mtia nia atajiorodhesha na kuandikisha taarifa zake.

3. Katika kutangaza nia, watia nia wanakumbushwa kuzingatia misingi ya maadili, utu na kanuni za uchaguzi za Chama chetu.

4. Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma imeagizwa kuhakikisha kuwa inatoa msaada kwa watia nia kujitangaza hasa kwa kuwaunganisha na vyombo vya habari.

Ado Shaibu,
Katibu Mkuu,
ACT Wazalendo.
30 Aprili 2020.
IMG-20200430-WA0343.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom