PCB inanisumbua naombeni ushauri

PCB inanisumbua naombeni ushauri

Soma kwa kukariri mdogo wangu halaf endelea kuelewa taratibu, piga msuli mwingi, concentrate achana mishe za mtaani. PCB ukizingua kidogo tu unakosa chuo
 
Kazana
Mbona mim dactar wa umeme na nimefaulu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nikajua unaongelea
Polychlorinated biphenyl

PCB
 
Acha ku postcJF soma. Sisi tulijuinga huku after Degree.
 
Shida ako kupata ajila mapema kijana Pambana c ulitaka sifa ety ooh kasoma na kuajiliwaa haahaha
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Kwa hiyo wewe Organic ulibahatika kufundishwa na wote, Ngaiza na Issue boy?
Nilisoma kwa Issue Boy ila walokuwa wanasoma kwa Ngaiza niliwaonao, tulikubaliana Issue Boy anafundisha concepts vizuri kwa muda mfupi. Ngaiza anaingia very deep alafu likizo inavyokuwa fupi hamalizi topic. Labda ukisoma kwa Ngaiza uvute likizo ikiisha ubaki. Organic na Inorganic huwa zinasomwa kwa likizo fupi
 
Somo la kemia kwa A_level siku hizi limekuwa jau kwa wanafunzi wengi sijui kwa nini hii hali.
 
Kemia tena? Mimi physics ndio ulikuwa mtiti.
Anyway tafuta washikaji hapo skuli walio vizuri chemistry upige nao collabo.Mm nimefundishwa organic na mshikaji and Trust me ilinipa B moja ya jeshima final shule nzima tulikuwa wawili wenye B.
Komaa ki mbinu na kijuhudi
Then road to Muhas
 
Siku hizi kuanzia Diploma ni rahisi ila kimbembe kuvuka dip uende Digrii kama huna hela utabaki C.O maisha yako yote.
Waliokuwa wanaibuka na kutoboa ni mbinu walikuwa wanakosa. Wengine uwezo mdogo sijui wanasahau haraka, kusoma kwingi mambo wanayo machache ila wanazingua.

Hiyo kubadili combination sikubaliani maana kasema somo moja linamsumbua. Wanabadili kama anaona nyota masomo mawili au yote. Then kwa wakati huu sidhani kama ni sahihi kuanzia udaktari diploma, atatumia nguvu nyingi mno. Bora akomae kwa kubadili mbinu kwanza.
 
Ha ha ha
Dakitari unafeli wapi?
Acha kushinda jf ule msuli.
 
Form Five muda bado unao. Likizo yenu inaisha sijui uko mkoa gani unasomea na unakuwa likizo wapi. Ungepiga papers za kujiinua na tuitions za kukubeba kama walimu hawako vizuri sana shuleni. Kama walimu wako poa ila wewe ndio huelewi piga disc na watu wanaojua afu kuwa na vitini vyako unavyotumia wala usichanganye materials.

Mimi nilisoma kwa Issue Boy (Josephat) Biology na Chemistry kisha Mgote Physics. Organic nilisoma ya Ngaiza imejaza kila kitu afu Inorganic nilisoma ya Issue Boy. Yani ukichanganya madesa hutoboi utachanganyikiwa. Kuna muda nilikuwa sisomi notes za mwalimu ambaye alikuwa vizuri sana kwa vile nishasoma kwingine, kwake nafanya mifano aliyotoa nikiipiga nishamuelewa, nisipoelewa najua nalag behind. Unaweza soma sana afu kumbe tactics mbovu.

Ni kawaida sana kukata tamaa ukiwa A level. Ila ni kawaida sana tena sana kupindua meza, hili wengi niliona waliweza. Jiulize una mademu, shule mnabanwa au mnazurula mitaani, unalewa au kuvuta, unashiriki makandokando kama dancing, kuwa mtumishi kupitiliza au mpira. Punguza baadhi ya vitu vinavyokula muda.

Usiwe na mkumbo wala kujilinganisha na watu kwenye kipato, uwezo kiakili, muda wa kusoma na mengine. Pia kuwa emotional stable, sio leo umeachika kwa Winnie mara Jane anakuzingua, kesho umekamatwa na simu au umetoroka ukaitwa kwa discipline master. Zoea kwenda dini ila usifie uko, kuna majinga yalikuwa yanalala kanisani eti yanalinda vyombo.

Ningeshauri mengi kama ningekuuliza kwanza afu nikajua situation. Ila hapa nimepiga kiujumla. Mimi nilikuwa na kasoro ila zilikuwa zinazidiwa na mchanganyiko wa mambo mazuri mengi.

Mandia katika ubora wake
 
Nilisoma kwa Issue Boy ila walokuwa wanasoma kwa Ngaiza niliwaonao, tulikubaliana Issue Boy anafundisha concepts vizuri kwa muda mfupi. Ngaiza anaingia very deep alafu likizo inavyokuwa fupi hamalizi topic. Labda ukisoma kwa Ngaiza uvute likizo ikiisha ubaki. Organic na Inorganic huwa zinasomwa kwa likizo fupi
Kwa comment hii sasa nimemwelewa Van De Beek alivyosema kwamba organic ya issue boy ni organic ya wavivu. Na nimekuelewa wewe pia kuwa unapima uzuri wa mwalimu katika ufundishaji kwa kuwahi kumaliza topic.
 
Piga kwanza kitabu, iache dunia kwa muda utaikuta tu dogo
 
Kwa comment hii sasa nimemwelewa Van De Beek alivyosema kwamba organic ya issue boy ni organic ya wavivu. Na nimekuelewa wewe pia kuwa unapima uzuri wa mwalimu katika ufundishaji kwa kuwahi kumaliza topic.
Huwezi elewa hizi mambo kama hujasoma. Unakuwa na likizo ya 3 weeks unaenda kwa Ngaiza anakupigia Organic anafika nusu wakati kwa Issue Boy anapiga kama 78%, ukivuta wiki moja tu kwa Issue Boy unaimaliza Organic kisha unaenda shule na visingizio vya kuumwa. Mimi niliyemaliza topic kwa concepts zote vs aliyefika 70% ya topic tukikutana class na mwalimu wa somo akaongeza kufundisha unahisi nani atakuwa competent?
 
Siku hizi kuanzia Diploma ni rahisi ila kimbembe kuvuka dip uende Digrii kama huna hela utabaki C.O maisha yako yote.
Uko anaenda kutumia nguvu nyingi kuliko hapa ambapo kabakiza mwaka mmoja. Akikomaa mwaka anakuwa amefanya kilekile ambacho atatakiwa afanye miaka 3 au 4 kama atakata tamaa kwa sasa.
 
Huwezi elewa hizi mambo kama hujasoma. Unakuwa na likizo ya 3 weeks unaenda kwa Ngaiza anakupigia Organic anafika nusu wakati kwa Issue Boy anapiga kama 78%, ukivuta wiki moja tu kwa Issue Boy unaimaliza Organic kisha unaenda shule na visingizio vya kuumwa. Mimi niliyemaliza topic kwa concepts zote vs aliyefika 70% ya topic tukikutana class na mwalimu wa somo akaongeza kufundisha unahisi nani atakuwa competent?
Mwalimu mzuri aliye deep hawezi kumaliza organic yote kwa week tatu labda awe anafundisha saa 5 kwa siku! Mwalimu mbovu aliye shallow ndo anaweza kumaliza organic kwa muda huo. Fuatilia hata walimu wakongwe kama Mkandawile uone wanafundishaje.
 
Daktar wa man u [emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119][emoji119][emoji2365]
 
Ni kweli siku hizi kusoma C.O ni rahisi ila shida kuvuka hatua nyingine vigezo vimeminywa sana ....nimesikia mtu wa Clinical Medicine kwa sasa haruhusiwi kusoma hata Dental ...asome MD tu na kozi zingine ila Dental akitaka aanze Diploma au apply na form six na bado huko MD kupata ishu maana waombaji wengi mno kama huna hela ya kusoma private imekula kwako.
Uko anaenda kutumia nguvu nyingi kuliko hapa ambapo kabakiza mwaka mmoja. Akikomaa mwaka anakuwa amefanya kilekile ambacho atatakiwa afanye miaka 3 au 4 kama atakata tamaa kwa sasa.
 
Kwa comment hii sasa nimemwelewa Van De Beek alivyosema kwamba organic ya issue boy ni organic ya wavivu. Na nimekuelewa wewe pia kuwa unapima uzuri wa mwalimu katika ufundishaji kwa kuwahi kumaliza topic.
ulijua natania......
Organic ya issue boy ni ya wavivu
 
Back
Top Bottom