Mcharo son
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 4,718
- 3,804
NI YA HUYO WA PILI KWA KUTOMALIZA TENDA. wa kwanza anawezakuwa na kosa la ufuatiliaji na kumchagua mzabuni mbabaishajiHv makosa ni ya mlipaji au mlipwaji
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NI YA HUYO WA PILI KWA KUTOMALIZA TENDA. wa kwanza anawezakuwa na kosa la ufuatiliaji na kumchagua mzabuni mbabaishajiHv makosa ni ya mlipaji au mlipwaji
Waziri wa Mambo ya ndani Charles Kitwanga amekana kuhusika kabisa na kampuni ya Lugumi ambayo kwa sasa inakabiliwa na kashfa nzito ya rushwa na uhujumu uchumi ambayo ilipewa tenda ya kufunga vifaa vya kuchukulia alama za vidole kwenye vituo vyote vya polisi kwenye Wilaya zote nchini na kushindwa kukamilisha tenda hiyo.
Juhudi mbalimbali zinazofanywa kuujua ukweli wa sakata hili umepelekea taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini(TAKUKURU) kutoa tamko la kuifungulia kesi mahakamani kampuni hii ya Lugumi pamoja na jeshi la polisi na kufanya uchunguzi wa kina wa sakata hili.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) imewaita bungeni IGP pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo watakuwa na kikao leo bungeni Dodoma na baadae baada ya kikao hicho ndipo wataweza kuongea na waandishi wa habari kuhusu suala hili.
Unaota wewe!Shanba la bwana kheri, mbuzi waliokula mazao ni wa bwana kheri, akida ni bwana kheri. HAKUNA KESI HAPO
Watasema swala liko mahakamani ili lisijadiliwe bungeni halafu Kesi itaondolewa na DPP mchezo kwisha na Watanzania tunavyosahau kwa haraka tukihoji tu... Wanazua ule Mchongo wa Escrow ya Stanbic kisha Lugumi anawekwa kando tukihoji Ile wanarudi na hukumu ya EGMA tunasherehekea baada ya miezi miwili jamaa wanaenda kufagia posta kisha yanakuwa huru. Basi mwaka unakuwa umeisha tunajipanga kwa season nyingine na nchi ndo inakuwa inasonga hivyo.
PCCB hawana jino la kwenda mahakamani, wao wakichunguza hupeleka faili kwa DPP ambaye huamua kufungua kesi mahakamani.
Yaani Jeshi la Polisi kushitakiwa na TAKUKURU??
Na Jeshi la polisi likikaidi kwenda mahakamani, ni kina nani watatumwa waende wakalikamate hilo jeshi la Polisi? Polisi haohao??
Naomba kujua kati ya kamati Ulinzi na PAC, ni ipi inahusika na mambo ya polisi?
Halafu huo mkataba wa Lugumi ulisainiwa mwaka 2011 kwanini kamati isimwite IGP wa wakati huo?
Hv makosa ni ya mlipaji au mlipwaji