PCCB WATAKA MAHAKAMA YAO, inawezekana?

PCCB WATAKA MAHAKAMA YAO, inawezekana?

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,537
Reaction score
6,472
JAMANI, nimesikia kwenye magazeti kuwa Dr. Hosea ametoa pendekezo kuwa, PCCB waundiwe mahakama yao binafsi, itakayo dili na kushitaki wala rushwa tu. niliona kama hilo ni pendekezo zuri, lakini, why only rushwa? na je? mahakama za tz hizi za kawaida zimeshindwa? hadi waundiwe wao mahakama yao special? na je?, kama corruption in general kama one of the organised crimes, je, ikiundwa mahakama ya rushwa, makosa mengine ya organised yapelekwe wapi:

makosa hayo ambayo yanaendana na corruption ni kama money laundering (usafishaji wa pesa), terrorism, piracy, human trafficking and smuggling and all other sorts of mafia dealings.....

PENDEKEZO LANGU NI KWAMBA, PCCB hadi sasa hawajaonyesha uwezo wowote ule wa manpower au hata experience kuwa na mahakama yao binafsi, na sio special sana wao kuwa na mahakama ya rushwa tu tukaacha izo organised crimes zingine. NAPENDEKEZA KAMA KUNA MAHAKAMA NYINGINE MPYA INAYOUNDWA BASI IUNDWE MAHAKAMA INAYOSHUGHULIKIA ORGANISED CRIMES TU, makosa yafuatayo:

  1. corruption
  2. money laundering
  3. human trafficking and smaggling
  4. terrorism
  5. piracy etc
kwasababu mara nyingi mtu anayefanya kosa la rushwa, lazima kwenye kosa lilelile anasafisha pesa (money laundering), anayefanya human trafficking, mlemle kwenye process kuna rushwa, haya makosa yanategemeana.

tatizo lililopo ni kwamba, ili kesi yeyote ile ya PCCB iendelee, ni lazima wapate consent ya DPP, ndio maana wakichunguza kesi, wanapeleka jalada kwa DPP, anasoma halafu anawapa kibali cha kuendelea. why hadi kibali cha DPP? kwasababu PCCB sio state attorneys (mawakili wa selikali wanaosimama badala ya serikali) ila ni ordinary persons ambao wanatumia mgongo/kibali cha DPP ambaye ni wakili wa serikali kushitaki baadhi tu ya makosa yaliyoko kwenye sheria yao tu na si kwenye sheria zingine.

Tatu, inasemekana hata uwezo au experience ya kuendesha mashitaka ni ndogo kwao, kesi ngapi wameshinda hadi sasaivi? na zaidi ya yote, hata zile za epa pale kisutu, wanawategemea state attorneys toka kwa DPP ambao wameacha majalada yao ya kawaida wakaja kuwapiga tafu pccb ili kuendesha kesi za pccb. AMINI USIAMINI, WAKILI YEYOTE WA KUJITEGEMEA KATIKA MAHAKAMA YEYOTE AKIONA PROSECUTOR NI PCCB HUWA ANASHANGILIA AJABU kwasababu anajua anaenda kushinda kesi.

siongei kuwaponda, lakini naomba serikali ijaribu kufikiria hili, either to empower pccb kiuwezo wa kuendesha kesi, na kama wanaunda mahakama yao basi, ibadilishwe sheria ili kesi watakazoendesha zisiwe zina stick kwenye sheria yao ya 2007 tu, bali hata sheria zingine na mahakama hiyo isiwe special only for corruption, but also for money laundering, and other trans national or national organised crimes.....I hope nitasomeka kama sitapigwa mawe hapa.
 
waanze kufanyia marekebisho sheria zao kwanza zina mapungufu mengi sana,hata mimi kajamba nani nina uwezo wa kujikwamua ktk kesi za rushwa kwa kutumia sheria zao hizohizo,mahakama hazina shida kabisa wajipange tu.
 
Actually nilisikia pia kitu kama icho. Tunaomba msituondolee tonge mdomoni sisi mawakili wa kujitegemea,....huwa nafurahi ninapoona pccb prosecutor anatetemeka mahakamani, authorities hana, na kwasababu hawaji mahakamani kila siku hawana uzoefu na technique, kusema ukweli, ni tofauti kabisa na mawakili wa serikali, wamepitwa mbaaali. Pale kisutu nimeona wanajiunga na mawakili wa serikali, ila wakiwa mahakamani hawaongei kitu, yaani kesi zile zote mnazoambiwa wameshinda pccb mfano zile za epa, wameendeshewa na mawakili wa serikali....lakini kwasababu wote ni Republic, watajuana wenyewe. ila kwa faida ya taifa, pccb bado hawajajipanga vizuri kuwa na watu wa kuwaendeshea kesi zao. Labda kama wakipata hiyo mahakama, wawaibe mawakili wa serikali wahamie kwao. lakini hata hivyo, ilishawai tokea katika nchi yeyote duniani kukawa na mahakama special kama hiiii au tunaanza sisi...mahakama tu hizi za kwetu nchi inashindwa kuendesha, tuanzishe mahakama nyingine tena?...hahahaha.
 
nchi ngapi tz zimefanya icho kitu? au ndo tunataka kufanyia mazoezi? mahakama hizi zetu zimeboreshwa? wanasheria wetu wa serikali wamepewa mazingira mazuri ili wote wasikimbilie PCCB ambako actually ndo kwenye maslahi mazuri kuliko wao ambao hata kazi hawawezi wanawategemea mawakili wa serikali?
 
Hii ni changamoto kubwa kwa Serikali,wadau wa sheria,na watu wengine wote,wenye mwamko na sheria za Tanzania mbali mbali!!
Kuwa na mahakama yao ni ktu kisichowezekana kwa sababu mahakamani zilizopo tu za kawaida zina mapungufu mengi,kuanzia usimamizi mzuri,vitendea kazi na majaji,mahakimu,mawakili na waendesha mashtaka kufanya kazi kwa mazoea bila kujali weredi na intergrity!
Pia suala kabisa kubwa linaloumiza ni mapungufu makubwa ya Sheria ya Rushwa,kwanza ina lack enforciability,ngumu ku-investigate na ku-prosecute pia sababu prosecution inategemea na Ushahidi uliokusanywa....Kwa mtazamo wangu bado tuna kazi kubwa kuelekea katika mazuri tunayoyawazia hususani katika masuala ya mahakama!!Ni hayo tu kwa mchana wa leo

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
sidhani kama ni ngumu kupeleleza, kwanini unasema ni ngumu, unaweza kueleza zaidi kuhusu hili?
 
brother HUTE ni kutokana na nature ya makosa yenyewe ya rushwa yalivyo....nina practical experience kuhusiana na hii kitu na sio research tuuu,so amini hayo,kwa kirefu tutafutane tupeane meengi zaidi
 
brother HUTE ni kutokana na nature ya makosa yenyewe ya rushwa yalivyo....nina practical experience kuhusiana na hii kitu na sio research tuuu,so amini hayo,kwa kirefu tutafutane tupeane meengi zaidi
kwa siku hizi kwasababu hata electronic evidence inaruhusiwa as per section 40A of TEA, ni rahisi mno, sema tatizo moja tu ambao pccb wanalo ni kwamba, when they arrest hawajui kuchukua cautioned statement vizuri kwaajili ya kutender. ila kama mtu ameiba, akapitisha hela bank, kwenye mpesa etc, ushahidi wake ni mzuri mno. sheria iko imara, na ni rahisi kuthibitisha. nimeshaendesha hizo kesi za pccb kwa kitambo kabla sijaacha kazi ya state attorney.....hivyo naongea kitu nilichofanya. na tunaposema mapccb ni mbumbumbu wa kuendesha kesi tunaongea kwa jinsi tulivyokuwa tunawaona wanavyotunyonya, hata kuahirisha kesi kwao ni ngumu wanataka hadi state attorney awepo, peke yao hawawezi, je, hiyo mahakama ikiwepo ndo si kitakuwa kichekesho?
 
Hapo ni kuhusu prosecution,ujue kabla ya mashtaka,kuna ku-arrest,ku-investigate na ndio mashtaka,sasa kesi za Jamaa hawa upelelezi wake ndio unasumbua

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
kwanza, dunia nzima siku hizi wanatengenisha investigation, arrest and prosecution. you the same person/body cannot investigate, arrest and prosecute halafu ukafanya fairness. ndio maana hata hapa tz kuna utaratibu karibia unamaliza tz nzima kwa polisi kuacha kuwa waendesha mashitaka, wao wabaki na investigation and arrest tu, na waendesha mashitaka wawe state attorneys. in order for the right to be done and be seen to be done, pccb hawatakiwi kabisa hata kwenda mahakamani labda kama mashahidi, hawawezi kukamata na kupeleleza wao wenyewe na kuprosecute, lazima watalalia upande wap/kuwa biased.....another body needs to come prosecute that case.

huu ndio utaratibu ambao dunia nzima unafuata kwa sasa, na sijui Hosea amepata wapi hilo wazo bila hata kuwauliza hao wazungu wafadhili wake wanafanya nini kwao. wazungu wanaompa misaada hosea kuendesha hicho kituo ndio hao hao wana encourage separation between prosecutors and investigators/arresting bodies. what do you think about this?
 
takukuru wanadai kwamba DPP ndo anachelewesha au ndo anakwamisha washitakiwa wa kesi mabalimbali kufungwa au kufikishwa mahakamani kutokana na sababu mbalimbali kama vile kuchelewesha kwa uchunguzi hvyo la Muhimu ni Takukuru kuwa na Mpitia Mafaili ya kesi zao baadala ya DPP na uchunguzi wafanye wao wenyewe.
 
Tatizo ni kwamba, tatukuru ni wabovu kuchunguza kuliko hata polisi, na pia PCCB wanakula sana rushwa wao wenyewe ndo maana kesi hazishindi, zile zinazoshinda ujue wameendesha kwa msaada wa mawakili wa serikali na ndio walioongoza na kuelekeza nini kichunguzwe.

amini usiamini, kuna vipengele vingine kwa mfano vya ku tender cautioned statements, yapo mapungufu mengi sana pccb wanayo na statement za pccb huwa si rahisi sana kuingizwa mahakamani kuliko zile za polisi. nawapa big up polisi hakika.

pia, kuna kesi nyingi sana huwa hazina umuhimu wowote na DPP/mawakili wa serikali wanaona kuwa, hata tukiendelea nayo hatuwezi kushinda....hivyo wakipeleka jalada pale, huwa linarudishwa, au wanaelekezwa kitu gani cha muhimu wameacha kupeleleza wakakifanyie upelelezi kwanza ndio jarada lirudishwe. na wapelelezi wengi wa pccb ni wabovu, hawaelewi sana what's going to be happening in court kulingana na kile wanachopeleleza, wao wanafanya kama research tu halafu wanapeleka jalada. I HAPPENED TO WORK AT DPP'S OFFICE for a long time, kabla sijaacha na majalada yao mengi sana nimeyafanyia kazi.

UGOMVI UKO WAPI? pccb ukiendesha kesi, unapewa promo ya fungu, ukiendesha kesi hadi mwisho uwe umeshinda au hujashinda unapewa kifuta jasho. imagine if you have many cases fungu utakalopata.....hahaha,sasa hawa jamaa wakileta jalada pale, likarudishwa kwamba waende wakapeleleze kitu fulani, au tukiwaambia kuwa kesi hii haina mashiko tutapoteza tu hela ya serikali kuiprosecute hivyo ifutwe, wanachukia sana kwasababu wamenyang'anywa tonge mdomoni.

after all, kesi nyingi ambazo wanang'ang'ana ni kama za ubadhilifu wa maafisa watendaji wa vijiji, na aina ya kesi za kuku kama hizo...ndo unaweza kuona wameng'ang'ania hadi wameshinda, ila zile ambazo mtu ataweka wakili wa kujitegemea kama za mamia ya mamilioni, hawana uwezo wa kuendesha, hata kupeleleza wanaharibu sana kesi.

huwezi amini ,wakati niko wakili wa serikali, kati ya majalada mengi niliyoandika, nimeshakutana na kesi nyingi sana wamepoteza vielelezo, au pale walipoenda kukamata mtu wameacha vile vielelezo vya muhimu ambavyo ndo vinge prove case, unategemea kesi itashinda hapo? NA JE? UNAWEZA KUPELELEZA, KUKAMATA WEWE MWENYEWE NA KU PROSECUTE na haki ikatendeka kweli? si utakuwa unafanya juu chini kuhakikisha umeshinda kesi hata kama si halali?...kwanini majukumu hayo yote yawekwe kwa mtu mmoja, patatendeka haki kweli hapo?

na wabunge waliohongwa hela na HOSEA wameongea bungeni hata hawajui jinsi mambo yalivyo.
 
Naungana na wewe hasa upande wa kusisitiza Kuimarisha PCCB...Kwa misingi ya Utawala wa Sheria na Usawa mbele ya sheria si vema kabisa Taasisi hiyo hiyo ifanye upelelezi,Ikushtaki na hapohapo iwe na Mahakama yake kwa kweli Rule against Bias itawabana kama wanasheria wanavyosema kwamba A MONKEY CAN NOT JUDGE AN AFFAIR OF THE FOREST...

Ni muhimu pia tuangalie kama Mahakama zingine zilizo anzishwa zimefanikiwa mfano;
  1. Mahakama Kuu ya Aardhi na Mabaraza ya Aardhi na Nyumba ya Wilaya(Changamoto ni kubwa na uhaba wa watenda kazi pamoja na miundombinu mingine migogoro ya ardhi ndo kwaaanza inaongezeka na kesi zinachukua muda mrefu.
  2. Mahakama Kuu kitengo cha Kazi na Tume ya usuluhishi (Japo inajitahidi kukimbizana na muda lakini bado)
  3. Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara(Gharama zake ni kubwa na Kiuhalisia licha ya kwamba inafanya kazi zake vizuri na kwa uwepesi gharama yake siyo rafiki kwa watu wa kipato cha chini
  4. Kuna Tribunals kama za Fair Competiton,PPRA,Tax Appeal Tribuna nk zingine zinaongozwa na Majaji wastaafu au majaji wengine ambao tayari wana mizigo mizito ya Kesi katika Mahakama zingine.
Kwa maoni yangu PCCB wapewe Mamlaka Kamili ya Kuendesha Mashtaka yanayo husiana na Sheria ya Rushwa na wasilazimishwe kuomba ridhaa ya DPP.Kuhusu msaada wa waendesha Mashtaka kutoka kwa DPP ni jambo la kawaida na sidhani kama linahusiana na upungufu wa ueledi kwa wanasheria wa PCCB kwani hata DPP hana waendesha Mashtaka mikoa yote hivyo wakati mwingine huwatumia State Attorney ambao wako sehemu husika.

Changamoto ya uendeshaji Kesi itapungua iwapo sheria itakataza kabisa kukamata watu na kuweka vizuizini bila kukamilisha uchunguzi hivyo kupunguza mlundikano wa Kesi ambazo nyingi ni kutajwa kwa kisingizio cha upelelezi haujakamilika
 
hapo kwenye red, state attorney ni maafisa katika ofisi ya DPP. dpp mwenyewe ni state attorney, ila ni bosi wa ma state attorney katika kitengo cha prosecutions. he's just one of the many directors the office of AG has. pale Attorney general office pale kivukoni front, kuna directors wengi na wote ni state attorneys. ni kweli mastate attorneys hawajasambaa sehemu zote tz na wanasaidiwa na police public prosecutors. kwa kifupi ni kwamba, hata waendesha mashitaka wa police ambao wako appointed by the dpp wanaweza kuendesha kesi vizuru kiliko hata pccb officers. naungana na wewe sana juu ya kutotakiwa kuwa na mahakama mahsusi ya pccb.

tatizo lililopo ni kwamba, uliposema kuwa pccb wasihitaji ridhaa ya dpp kuendesha kesi, you cannot have two directors of public prosecutions in the same country. haijawahi tokea kwenye nchi yeyote ile na italeta mgongano sana kwasababu, ukisema mmoja awe director wa makosa ya rushwa tu, makosa ya rusha hayako independent, ndani ya rushwa utakuta kuna makosa mengine mengi sana ambayo yataingilia kabisa mfumo wa kuwa na mkurugenzi wa mashitaka. mfano: kwa sheria ya pccb no. 21 ya 2007, makosa mengi sana ya corruption, sijui embazzlement, abuse of position etc, yanaingiliana sana na makosa mengine ya jinai yatakayohitaji kushitakiwa katika penal code (na wao kipindi hicho watakuwa hawatakiwi kutumia penal code, bali sheria yao tu? impossible), huwezi tenganisha. palipo na money laundering, lazima pana ka aina ya corruption, abuse of position, conspiracy, human trafficking and many other trans organised crimes. ningekubaliana na wewe kama ungesema kuwa, ndani ya ofisi ya dpp, kuwepo kitengo maalumu cha kushugulikia rushwa tu, na, hapa nasisitiza, OFISI YA DPP INATAKIWA IJITEGEMEE KUTOKA KWA ATTORNEY GENERAL, dpp anapoendelea kuwa chini ya attorney general hawezi kuwa na kitengo pekee kwaajili ya hili na akafanikiwa.

kwamfano, pale kwa dpp kwa sasa kuna kitengo cha asset recovery na money laundering, hiki kinashugulikia kurecover assets ambazo zimepatikana pasipo halali, na kitengo hiki ndicho kinachowasaidia sana pccb kuendesha kesi zao hata hizo za hapo kisutu. kuna madogo funali wapo pale nawajua. kingewepo kitengo kingine pekee cha corruption, human trafficking etc,....

ili pccb wasiwe na ridhaa ya dpp kuendesha kesi, lazima iwekwe kwenye katiba, kasababu dpp ni creature of the constitution, dpp ametajwa kwenye katiba uteuzi wake na kazi yake, hivyo labda na pccb mkurugenzi wao atajwe mle ndio apate power. nafikiri ni kitu cha process na inawezekana.
 
Back
Top Bottom