Car4Sale PDF: Jumla ya Gharama za Kuagiza Baadhi ya Magari kwa Mwaka 2021

Ni muhimu kufahamu maana wengine wana promote hivi unafanya nao biashara mzigo ukifika unashangaa kuna utitiri wa kodi zingine za ziada unatakiwa kulipia... ambazo hukuambiwa mapema...
 
Ni muhimu kufahamu maana wengine wana promote hivi unafanya nao biashara mzigo ukifika unashangaa kuna utitiri wa kodi zingine za ziada unatakiwa kulipia... ambazo hukuambiwa mapema...

Umeuliza swali la msingi sana, jamaa ameshasema hapo ni gharama za uwakala, ushuru wote, bandari, uchakavu, usajili, documentation hadi namba ya gari. Hapo ukishaichukua unaingia peterol station unpiga full tank kwanza kusuuza tank...
 
Mbona kama Bei zimepand au ndio kifaida.
 
Huna unachojua apa kaweka makadilio tu ila inategemea na mwaka wa gar inaweza panda ama shuka...
Kwa taarifa yako ilibidi aweke price range maana unaweza kununua gari ya mwaka mmoja lakini bei zikapishana hata milioni 3 kwa tofauti ya kilomita ilizotembea au accessories zilizofungwa. Pia kuna gari inaweza ikawa ilipata hitilafu ikauzwa bei ya chini kuliko nyingine

Mfano unasema IST old milioni 13, vipi kama imetembea kilomita 20,000 itauzwa bei hiyo?
Unasema sina nachojua, umejuaje kama sijui? kwa kuweka fixed price kwa gari za aina fulani ambazo ni used ni very poor marketing strategy. Zingekuwa ni brand new sawa. Najua kwa elimu yako ndogo huwezi kunielewa ila nakupa tu mfano tembelea site zote duniani za vitu used uone kama bei yake ni moja. Anza na makampuni makubwa ya magri used uone jinsi bei zinavyotofautiana utaelewa nachosema

Kwa jinsi tu bei zilivyowekwa mtoa mada inaonekana ana mtaji ila hana shule au kama shule ipo basi anataka kuwapiga watu

Hamkeni watanzania ukosefu wa elimu unatugharimu sana
 

[emoji419][emoji375]
 
hivi hizo gari namba 43 zina kitu gani kinachofanya ziwe nyingi hapa daslam
 

Sawa asante
 
Talking out of ignorance en envy.....!!!!!
 
Kaweka na faida kubwa ukienda beforward unapata chini ya hapo
Befoward siku hizi bei zao zimechangamka kiasi.

Kimwomwe wana scheme ya kulipa kidogo kidogo ndani ya muda fulani.
 
Brother Mimi nimekuelewa,
Ila nilichowaza bei ikitofautiana inakula kwenye profit yake. Yaan yeye ana maintain sales price yake (constant) ila profit yake ndio inabadilika.

Yaan mfano Kama gari ya 13mil ye anapata profit ya 1.5mil (total cost kwake 11.5mil) Basi ikitokea gharama zikazid kwake mpaka labda 12.5mil basi atakula only laki 5 profit.

Na ikitokea ameipata kwa pungufu labda imemgharimu total 10mil bas atapiga profit ya 3mil.
 
Umeuliza swali la msingi sana, jamaa ameshasema hapo ni gharama za uwakala, ushuru wote, bandari, uchakavu, usajili, documentation hadi namba ya gari. Hapo ukishaichukua unaingia peterol station unpiga full tank kwanza kusuuza tank...
Service je?Utaendesha bila kufanya service?
 
Sidhani kama mfanyabiashara anaweza fanya kitu kama hicho. Anyway nilipose hiyo challenge ili tufungue mjadala. Humu JF tunajifunza ingawa mtu uki-challenge unaonekana kama unamharibia biashara lakini lazima tufundishane ili twende sawa na dunia ilipo.

Ukichukulia positive kitu unachoelekezwa unaweza ukapata elimu nzuri sana zaidi ya darasani. Kwenye biashara ya vitu used huwezi kuwa na bei constant kwa kitu cha aina moja kwa kuwa bei inatokana na kilivyotumika. Gari inaweza kuwa ya 2004 ila toka inunuliwe imetembea km 15,000/= hivyo bei yake itakuwa expensive kuliko same vehicle iliyotembea km 200,000/=

Ingekuwa 0km unaweza kuweka constant price

Factors zinazo determine price kwenye kitu used ni nyingi kama cc, km, uchakavu wa body nk. Ukiingia kwenye mitandao mikubwa ya magari used utaona gari say Prado ya 2014 moja inauzwa bei fulani nyingine iko juu kwa usd 3000 zaidi. Hii inatokana na factors nilizozitaja hapa juu. Sasa leo mtu anakwambia bei ya gari used aina fulani ni constant hapana haiwezi kuwa hivyo
 
Hizi garama ni mpaka nakabidhiwa funguo au CIF tu
 
Service je?Utaendesha bila kufanya service?

Tunaongelea umetoka kuchukua mchuma kwa muuzaji mwamba.

Hayo ya service si ukishaachana na muuzaji? Kwani hata kama unataka kufanya service hauruhusiwi kupiga full tank?

Service lazima uwe umeshaiendesha gari kidogo ujue na matatizo mengine ili ukienda service inaangaliwa vitu vyote kwa ujumla wake.

Ahsante
 
Nia yangu nilitaka kujua kama kwa mfano nimetoka kupokea gari kutoka beforward au kwa hawa jamaa, hiyo gari huwa inahitaji kufanyiwa service kabla ya kuendeshwa?
 
Nia yangu nilitaka kujua kama kwa mfano nimetoka kupokea gari kutoka beforward au kwa hawa jamaa, hiyo gari huwa inahitaji kufanyiwa service kabla ya kuendeshwa?

Mara nyingi gari inahitaji kuchekiwa. Kuna vitu kama tairi, bush, battery vinaweza kuwa miongoni kulingana na hali ya gari. Service ya gari ile ya kawaida muhimu sana. Lakini hayo unaenda kufanya wewe mbele ya safari.
 
KIMOMWEMOTORS naomba nitoe ushamba kidogo,ninapopokea gari kutoka kwenu natakiwa kuifanyia service gari hiyo kabla sijaiendesha,mfano kumwaga oil?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…