PDF la oil chafu hili hapa

PDF la oil chafu hili hapa

Biashara ya Oil Chafu

Biashara ya oil chafu ni biashara kubwa inayowaingizia watu mamilioni kwa mwezi, na vituo vikubwa viko maeneo yafuatayo:
  • Tabata Dampo
  • Temeke
  • Mbagala
  • Buza
  • Kigamboni
Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaosafirisha oil chafu mpaka nje ya nchi, hasa katika nchi za:
  • Zambia
  • Kenya
  • Uganda
Hii ni biashara isiyopenda utapeli, ghiliba, uongo wala udanganyifu. Kufanya hivyo ni kujitakia kifo cha mapema na cha fasta sana!

Udanganyifu ambao unavumilika uko kwa wakusanyaji na wasambaji wadogo, ambao huongeza maji na unga wa mfano ili kuongeza ujazo. Hawa kuna mbinu ya kuwabaini na kuwadhibiti.

Oil chafu rangi yake halisi ni nyeusi tii, inawaka haraka, na ina mlipuko mzuri.
Oil chafu iliyochakachuliwa inakuwa na weusi uliochakaa na haiwaki vizuri
Oil chafu iliyochakachuliwa ukiiwasha moto wake hupaparika hauna utulivu kabisa
Test nyingine ni kudondosha tone la oil kwenye karatasi nyeupe baada ya kuikoroga vizuri.. Kama ina maji basi kwenye lile tone kwenye karatasi kutakuwa na mduara wa unyevu.
Test ya mwisho ni kutumbukiza fimbo ndefu ndani ya tank na kuitoa.. Kama kuna maji utaona wazi mafuta yakijitenga na maji
Kwa kifupi hilo ndio faili zima la oil chafu.. Kama kuna niliyosahau ni madogo dogo
Mkuu naweza pata mawasiliano yako ili uweze kuniweka vizuri kwenye hii biashara.
 
Back
Top Bottom