wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 503
- 1,432
Kabla ya kuilaumu Rwanda kuhusu suala la M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), nataka nikupatie historia fupi kuhusu kinachoendelea katika sehemu ya mashariki ya Congo. Hii ilianza vipi?
Unachosikia kila mara ni kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23, na serikali ya DRC inapambana na waasi wa M23 ili kukomboa sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hayo ndiyo unayosikia kwenye habari kila siku. Lakini nataka nikuambie kilicho nyuma ya pazia kinachoendelea huko.
Twende nyuma kwenye chanzo cha tatizo hili. Wakati wa Mkutano wa Berlin Confeence enzi za ukoloni, Wakoloni walikuwa wanaigawa Afrika miongoni mwao, Wabelgiji walichukua Congo, Wajerumani walichukua Rwanda, Wajerumani pia walichukua Tanzania, na Waingereza walichukua Uganda na Kenya. Waligawanya maeneo haya bila kujali mipaka ya makabila.
Makabila mengi barani Afrika yaligawanywa kwa mipaka ya nchi, utakuta kabila moja linapatikana pande zote mbili za mpaka. Hili ni jambo la kawaida sana Afrika kwa sababu Wakoloni hawakujali wanavyogawanya makabila haya, Wahaya unawakuta Uganda na Kagera, Wakurya unawakuta Kenya na Tanzania, Wamakonde unawakuta Tanzania na Msumbiji, Wanyakyusa unawakuta Tanzania na Malawi.
Katika mgawanyo huu, kabila la Watutsi liligawanywa kati ya nchi mbili: Rwanda na Zaire ya wakati huo ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Sasa, kwa nini waasi wa M23 wanapigana dhidi ya majeshi ya serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa katika mashariki mwa Kongo? Na M23 ni akina nani?
Waasi wa M23 ni kundi la waasi lililoanzishwa na Watutsi wenyewe ili kulinda ardhi yao, ambayo ni sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Walijilinda dhidi ya nani? Dhidi ya serikali ya DRC ambayo imekuwa ikijaribu kuchukua ardhi yao kinyonyaji.
Labda unajiuliza, kwa nini kundi la watu linajaribu kujilinda dhidi ya serikali yao wenyewe? Ndiyo, hiyo ndiyo hali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hakuna utawala wa sheria. Kila mtu anajitafutia mwenyewe. Wanyonge hukosa ardhi na kusambaratishwa.
Mataifa Super power kama Marekani, China, na Urusi yameingia DRC na kuchagua maeneo wanayotaka kuchimba madini, Maeneo mengi yenye madini wenyeji huwa wanafukuzwa, kukiwa na upinzani wa wenyeji ndio unaweza kuyapa silaha makabila yanayoishi huko kupigana na makabila mengine yatayoleta upinzani, inapobidi jeshi hupelekwa ni mpaka serikali yenyewe inahusika.
Majeshi ya DRC mara nyingi hutumia mbinu za kuwahamisha watu wa maeneo fulani na kuruhusu makampuni ya Kimarekani, Kibelgiji, na Kifaransa kufanya uchimbaji wa madini katika maeneo hayo huku wakazi wa asili wa maeneo hayo wakisambaratishwa na kuwa wakimbizi, HICHO NDICHO WATUTSI WAMEKATAA !!
Hii ndiyo sababu Watutsi wa mashariki mwa Kongo walilazimika kujihami, kwanza kupitia Banyamulenge, na sasa kupitia M23. Katika DRC kabila lisilo na silaha ni kabila lililomalizika, hasa ikiwa linaishi kwenye ardhi yenye utajiri, Utafukuzwa ukileta kiburi unapigwa chuma.
Mashariki mwa Kongo ina utajiri wa madini kama uranium, lithiamu, na madini mengine yanayotumika kutengeneza simu, drones, na betri za magari ya umeme. Ndiyo maana mapigano yamejikita katika sehemu hiyo kwa sababu Super Powers wanataka kuchukua madini hayo lakini haijawa rahisi palewanapotaka kuwafukuza Watutsi wa eneo hilo kwa kutumia jeshi la Congo na vikosi vingine vinavyoaminishwa uongo kwamba maeneo hayo yametekwa na M23, lengo ni kuwatoa hao Watutsi wanaokataa kuhama.
Ndio maana watu wengi wamebaki midomo wazi kuona wakongo wa mahariki wakiserekea m23 walipoikamata Goma kwa muda, Ni wazi kwamba hata kushindwa kwa jeshi la Congo na vikosi vingine ni kwasababu ya kukosekana kwa ushirikiano na wananchi wa huko, wao wapo upande wa M23
Rwanda inaingiaje kwenye hili? Watutsi wa mashariki mwa Kongo waliomba msaada kutoka Rwanda kwa sababu wanashirikiana lugha moja, tamaduni moja, na dini moja. Rwanda chini ya serikali ya Watutsi, haikuweza kuwapuuza.
Zaidi ya hayo, baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Wahutu waliokimbia walijikusanya mashariki mwa Kongo kujaribu kurudi na kuipindua serikali ya Rwanda kwa nguvu. Hivyo, usalama wa Rwanda unategemea kuwadhibiti Wahutu walioko DRC. Rwanda inatumia Watutsi wa mashariki mwa Kongo kuzuia tishio hilo.
Serikali ya DRC wanafanya kazi kwa maslahi ya mataifa mengine yenye hamu ya kuchukua madini ya mashariki mwa Kongo. Umoja wa Mataifa pia unatumika kama kifuniko kwa unyonyaji huo.
SOLUTION
Huwezi kuwafukuza Wamakonde wa Mtwara waende Msumbiji bila ardhi, kama huwataki mega Mtwara ihamie Msumbiji na watu wake, it takes two to tangle ! sasa vuongozi wapo Kinshasa, wao wanataka wawafukuze watu huko Mahariki waende Rwanda, ila ardhi ibaki Congo! NI UONEZI !
View: https://x.com/Roel6825008/status/1883996837138555357?t=PS1N_WYp2FhC4v1gdIjlVw&s=19

- Ukiwafukuza wahaya wape ardhi yao waiunge Uganda au iwe nchi
- Ukiwafukuza Waha wape ardhi yao waiunge Burundi au iwe nchi
- Ukiwafukuza Wanyiha wape ardhi yao waiunge Zambia au iwe nchi
- Ukiwafukuza Wanyaki wape ardhi yao waiunge Malawi au iwe nchi
- Ukiwafukuza Wamakonde wape ardhi yao waiunge Msumbiji au iwe nchi
- Ukiwafukuza Wachaga wape ardhi yao waiunge Kenya au iwe nchi
- Ukiwafukuza Wamasai wape ardhi yao waiunge Kenya au iwe nchi
- Ukiwafukuza Wakurya wape ardhi yao waiunge Kenya au iwe nchi