PDF la vita inayoendelea DRC, wakongo wa Mashariki wanaonewa na serikali yao, wakombozi wao ni M23 na Rwanda

Hii vita ni ngumu mno kutatuliwa ..
Otherwise hiyo nchi igawanye upya..
Drc inataka kuwafukuza watusi Ilihali wamekaa goma tangu kale wanasingizia siyo wakongo
 
Sorry Tanzania ikianza kuwafukuza wahaya w bukoba je Uganda itawatetea? Kisa kuna wahaya pia Uganda?
KAZI ni kipimo cha UTU
Yaani anaeleta mada kwamba rwanda anaingia DRC kwaajili ya kusaidia watutsi ni ujinga mtupu inamaana leo tanzania inavyowaondoa wamasai ngorongoro kenya inaweza kuingilia kwasababu na kenya kuna wamasai.
Vitu vingine hata havina logic
 
Mkuu ni kweli kabisa mataifa kama US, UK, China, Russia watake hizo rasilimali kisha watumie mbinu kama hizo?
 
By the way umenifurahisha na nimepata kitu ulipoelezea kwamba mipaka ndani ya Africa zamani iliwekwa kutokana na ukabila.

Mifano uliyoitoa ni hai na inaakisi uliyoyazungumza.
 
Mwandishi umeandika ujinga wa kiwango cha mwisho nina uhakika hata wewe mwenyewe hukijui ulichokiandika
 
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAJE.
 
Dawa hapo, ni wakongo Watusi, wapewe ardhi Yao, wajitawale,
Au wwingize kwenye jeshi LA nchi,
Uwezi kuwafukuza Masai wa Arusha, waende Kenya, bila ardhi, kama uwataki, mega Arusha, iende Kenya na watu wake, sasa vuongozi wa Kinshasa, wao wanstaka wawafukuzewanyamurenge, Watusi wakongo, waende Rwanda, ila ardhi Yao, ibaki Congo! It's stupid! Ni sawa sawa, uwataki wahaya, unataka waende Uganda, ila kagera, ibaki TZ! Kama uwataki, wafukuze na ardhi Yao!
 
Point nzito hii, ndicho ambacho hata Nyerere alikishauri
 
💯%💐💐💐
 
Watanzania wengi wanalaumu M23 bila kwanza kujifunza ukweli wa tatizo, Congolese ukabila unawamaliza na M23 watapigana mpaka kieleweke
 
Kuna kitu hakisemwi....
Ni nani wanazifadhili pande zote mbili za mapigano?

Yani hao M23 na Kagame wao VS DRC na wanajeshi wao...

Naombeni majibu.. maana hao ndo washenzi na tukiwajua ndo tumemjua mchawi. Which Western Countries is on either sides!?

Alafuuu...hao Mnaowaita Watusi wa Eastern Congo wanawajibika kwa Nchi gani!? Yani huduma za kijamii ie shule, maji , umeme, masoko(exchange) , banks, saragu ipi wanatumia... Au ni ka nchi kenyewe kasiye na Baba wala Mama...

Naomba majibu.
 
Mtoa mada, M23 wanajilinda au wanataka kutawala Goma waunde mamlaka yao?
 

Japo uliyoyaandika, baadhi yana ukweli, lakini mengine pia umepotosha sana:
Nimefanya kazi mbalimbali nchini DRC.

Kwanza siyo kweli kuwa nchini DRC wananchi wanafukuzwa ili makampuni yachimbe madini. Sheria ya ardhi ya DRC inawapa mamlaka makubwa wananchi kuliko ilivyo kwa Tanzania.

DRC huwezi kuchukua ardhi yoyote ukachimba madini bila ya kukubaliwa na wamiliki wa ardhi ambao ni wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na machifu wao. Ili upate ruhusa ya kuchimba madini DRC lazima uwe kwenye terms nzuri na wananchi na machifu wa eneo hilo. Makampuni ya nje yanapoingia DRC, huwa na msululu wa vikao na mikutano kuanzia kwenye maeneo husika na majimbo. Serikali kuu haiwezi kutoa leseni ya uchimbaji madini bila ya kupata mapendekezo kutoka utawala wa majimbo.

Pili siyo kweli kuwa jimbo la North Kivu ambalo lipo Mashariki mwa DRC, ndiyo jimbo tajiri sana kwa madini kwa DRC. Majimbo ambayo yanaongoza kwa utajiri mkubwa wa madini ya Cobalt na mengine mengine mengi ni Lualaba na Haut-Katanga, ambayo yapo kusini kati.

Hata hivyo, ni kweli kuwa hata hilo jimbo la Kivu lina madini na mali nyingine asilia kama vile misitu mikubwa. Nchi ya Rwanda imekuwa ikiiba rasilimali za eneo hili kwa kupitia jamii ya watu wenye asili ya Rwanda, yaani kabila la watusi. Na Rwanda kwa kupitia jamii hii ya watusi imekuwa ikitamani jimbo hili lijitenge na kuwa sehemu ya Rwanda, na hiyo ndiyo sababu ya Rwanda kuanzisha kundi hili la wapiganaji wa M23 ambalo linapewa kila kitu kuanzia mafunzo, silaha mpaka maelekezo na nchi ya Rwanda. Kinachotkea Rwanda hakina tofauti na kinachotokea mashariki mwa Ukraine ambako Russia kwa kutumia wakazi wa Mashariki ya Ukraine wanaoongea kirusi, inataka kulichukua eneo lote la Mashariki la Ukraine.
 
ACHA UPUMBAVU.

KWAHIYO UNATAKA WAKURYA WA KENYA WAPAMBANE NA SERIKALI KULINDA ARDHI YAO?

HIVI HUU UPUMBAVU MNAANDIKA BAADA YA KULA NINI?
Kama serikali inataka kuwanyanyasa na kutaka kuwaondoa kwenye ardhi yao wanaweza kujikusanya kupambana na serikali yao.
 
Baada ya kusoma uzi wako na hiyo clip nakubaliana na unachotaka kusema.
Ni kweli serikali ya kigali inaweza kuwa inapambana na DRC Congo kujihami na wahutu waliokimbilia DRC ili wasije kujikusanya tena ili kuipindua serikali ya Rwanda.
 
Tshesekedi ameamua kuwa mkabila kama waliomtangulia, hivi inawezekana vipi leo uwaambie Banyamurenge walioishi Congo kabla ya partition of Africa leo waondoke na kuwaita watusi wa Rwanda na kuanza kuwaua, imagine unawaambia wamasai au wakurya warudi Kenya na kuanza kuwaua, ni sawa na kina Kagame walipofukuzwa na kuwa wakimbizi kwa miaka 50 huku wakiambiwa hamuwezi kurudi nchi imejaa, ni very simple solution acha ukabila na wahakikishie usalama wao, hizo story za M23 wanataka kuigawa nchi ni upuuzi mtupu na kumbuka Banyamurenge walishafanyiwa genocide na Congolese army na vikundi vya wahutu waliokimbia Rwanda, mambo nani anafadhiri nobody cares na hayataleta amani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…