PDPC: Taasisi zote ziteue Afisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi kabla ya 8 Aprili, 2026

PDPC: Taasisi zote ziteue Afisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi kabla ya 8 Aprili, 2026

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722


Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) imezitaka taasisi zote nchini kuhakikisha zinazingatia kikamilifu matakwa ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, ikisisitiza kuwa kutokufuata sheria hiyo kutasababisha hatua kali za kisheria.

Kwa mujibu wa Tume hiyo, adhabu kwa watakaobainika kukiuka sheria zinatajwa katika vifungu vya 60, 61 na 62, ambapo zinaweza kujumuisha faini kuanzia Shilingi 100,000 hadi Shilingi 20,000,000 kwa mtu binafsi, kifungo cha hadi miaka 10 jela, au vyote kwa pamoja.

Vilevile, taasisi zote zimepewa hadi Aprili 8, 2026 kuhakikisha zinatimiza masharti muhimu, ikiwemo kuteua Afisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi (DPO), kujisajili rasmi katika Tume hiyo, pamoja na kuandaa na kutekeleza sera na miongozo ya kulinda taarifa binafsi.

Maelekezo hayo yametolewa leo Alhamisi, Machi 26, 2026 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dkt. Emmanuel Mkilia, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Jambo TV
 
Kwamba taarifa za watu katikati taasisi Sasa zinakuwa accessable na DPO,

DPO wapewe ulinzi
 
😁😁 tusinyimane ridhikiii wajameni
lee daniels GIF by Empire FOX.gif
 
Back
Top Bottom