John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Hili wanatafuta trend tu na watu wajue kuna kitu kama hiki. Kuandika taarifa sahihi kuna saidia mambo mengi.
1. Pale upatapo changamoto unaweza saidika.
2. Ukisahau au kupoteza kitu ndani ya nyumba ya wageni unatafutwa na kurudishiwa kitu chako.
3. Kuna mamlaka zinachukua too mbalimbali za kiserikali huko kwenye nyumba za kulala wageni usipoandika watajuaje mmelala ili wakusanye tozo.
4. Issue za kiusalama kama wafanyavyo polisi na uhamiaji usiku kukagua vyumba na kujua uhalali wa uwepo wako nchini.
Katika hili, napingana nao ila nyie wazinzi ndio mnafurahia.
Binafsi nikisafiri kikazi huwa naandika taatifa za kweli kwenye kitabu cha wageni na huwa nakidaigi ili nisaini kitabu.
Zipo faida na hasara zake katika kufanya hivyo. Kwenye Nchi nyingi sana ambazo hakuna Demokrasia ya kutosha na Utawala wa Sheria kama hizi Nchi zetu za kiAfrika, jambo hili Lina hasara nyingi zaidi kuliko faida. Kama umeshawahi kufika na kulala Gesti, Lodge, au Hotelini katika nchi kama vile Zimbabwe, Rwanda, Urusi, na Nchi zingine zinazofanana na hizo, nafikiri utakuwa unanielewa vizuri Sana ninachomaanisha hapa.
Wale Watu ambao ni maarufu katika Jamii ndio wenye hatari kubwa zaidi kuhusiana na suala hili.
Nchini Rwanda kuna Watu wanaojulikana Sana na wenyeji wa huko wanaitwa kwa jina la "SEPO," na nchini Zimbabwe na pia nchini Urusi kuna Kitu kinaitwa "Operation Midnights."
So, take a great care to disclose your identity in those areas where you are there!