Pele aruhusiwa kutoka Hospitalini

Pele aruhusiwa kutoka Hospitalini

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1646133443058.png

Gwiji wa Brazil Pele ameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupata matibabu ya uvimbe na maambukizi ya mfumo wa mkojo.

Mshindi huyo Kombe la Dunia kwa mara tatu, mwenye umri wa miaka 81, alilazwa katika Hospitali ya Sao Paulo Albert Einstein tarehe 13 Februari, kwa ajili ya matibabu ya uvimbe wa utumbo mpana.

Siku nane baada ya kulazwa, madaktari waligundua ugonjwa wa mfumo wa mkojo, ambao uliongeza muda wake wa kukaa hospitalini.

Hata hivyo, hospitali hiyo ilisema Pele yuko katika "hali nzuri ya kiafya".

Ataendelea na matibabu ya uvimbe huo ambao uligunduliwa kwa mara ya kwanza katika vipimo vya kawaida mwezi Septemba.

Pele ni mfungaji bora wa muda wote wa Brazil akiwa na mabao 77 katika michezo 92, mshambuliaji huyo wa zamani ni miongoni mwa wachezaji wanne pekee waliofunga katika michuano minne ya Kombe la Dunia.
 
Back
Top Bottom