Pele kuzikwa ghorofani

kiumbempole

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2016
Posts
593
Reaction score
983
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Brazil, mwili wa Pele utaanza kuagwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Vila Belmiro wa Santos, baada ya shughuli za Luiz Inacio Lula da Silva kuapishwa kuwa Rais wa 39 wa Brazil, leoJumapili.

Pele atazikwa Jumanne, huku shughuli za mazishi ikielezwa zitafanana na zile za Malkia. Uwanja wa Vila Belmiro, unaotumiwa na Santos FC, timu ambayo Pele alitumikia kwa sehemu kubwa ya maisha ya mpira.

Uwanja huo ndiyo utatumika kwenye shughuli za mazishi Jumatatu na Jumanne. Santos historia yake haielezewi bila ya kumtaja Pele na ndiyo maana wamelichukua jukumu zima la mazishi yake.

Shughuli za mazishi zitadumu kwa saa 24, kuanzia Jumatatu hadi Jumanne, ambapo jeneza lake litapita mitaani na kupita mbele ya nyumba ya “O Rei’s” mama yake, Celeste. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Brazil, mama yake Pele amelala tu kitandani na anaripotiwa kuwa na miaka 100.

Kisha mwili wa Pele utakwenda kupumzishwa kwenye makaburi ya wima, Memorial Necropole Ecumenica. Ni familia tu ndiyo itakayoruhusiwa. Makaburi ya Necropole Ecumenica ni ya ghorofa.

Inaelezwa kwamba makaburi hayo yaliingia kwenye rekodi ya kitabu cha Guinness 1991 kuwa makaburi marefu zaidi duniani yakiwa yamejegwa kwenye jengo la ghorofa 14. Inaelezwa kwamba mwili wa Pele utapumzishwa kwenye ghorofa ya tisa. Mwanzoni jengo hilo lilijengwa ili kuwa makazi ya watu, kabla ya mwaka 1983 Pepe Altstut kulibadili na kuwa nyumba ya wafu.

Mwananchi
 
Ukitaka kufikisha ujumbe, jitahidi kuweka maelezo kamili yenye kubeba ujumbe wote...

 
Tutu alifanywaje tena vile? Sasa ni zamu ya Pele kutuletea maajabu. Kuna uzi niliwahi kuusoma hapa nadhani ni wa The bold. Huko mexico kuna makaburi ya hatari. Makasri kabisa ndio kaburi lenyewe.
Hao ni ma Don wenye hela chafu yaani kaburi lina thamani zaidi ya jengo

Ila haya ya kuwekwa kwenye jengo ni mpango wa kupunguza utumiaji wa ardhi na badala yake wanahofadhiwa kwenye vyumba maalum kama mortuary tu

Germany kuna makaburi yamefukuliwa kuna wafu wamegoma kuoza kwa mda wa miaka 40 wako vile vile
Huwa wanaondoa mifupa iliyobaki na kuichoma ili wazikwe wengine sasa wamekuta bado wapo tu

Duniani kuna maajabu sana huko India vultures ndio walikuwa wanalishwa maiti

Israel pia wana makaburi ya kwenye majengo kwa ajili ya ardhi haitoshi
 
Duh
Dunia ina mambo!


Kwahiyo wanaozea humohumo
Na je familia ikitaka tembelea kaburi la mpendwa wao, ndio wanaliona kiupande upande tu?

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Yaani we acha tu
Wanaozea humo na wampendwa wanakuja kusalimia kama ziara za makaburini tu

Mimi kuna aina mbili Tatu za kuwaaga wapendwa ndio zimenishangaza

Huko Japan na Arizona [emoji631] kuna watu wametengeneza freezer kubwa za kuhifadhi maiti milele yaani unagandishwa milele na bei yake ni $200,000 wapo waliolipia kabla ya vifo vyao waki secure space

Na huko Tibet hao ndio kiboko maana ardhi yao ni milima na mawe matupu hakuna pa kuzika

Mfalme mmoja miaka mingi iliyopita akataka maiti ziliwe na Ndege waitwao Vultures hao wanakula kila kitu

Kuna watu ndio kazi yao unawapa mpendwa wako nao wanaanza kukata kata na kuwatupia vultures
Ningeweka picha ila sio vizuri

Kama una moyo kaangalie YouTube sky burial ceremony
Usiseme sijatoa onyo
 
Duh but why
Wengi wao wanakuwa wanaishi maeneo ya karibu na hakuna sehemu za kuzika karibu
Wamepunguza matumizi ya ardhi kwa mambo mengine badala ya makaburi

Yaani majengo na viwanda ni bora kuliko maiti kwa sasa

Hata bongo wamefukua makaburi 1500 kwa kupisha Reli ama
Yaani Dunia hii sijui tunaenda wapi scary [emoji32] [emoji15]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…