Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Brazil, mwili wa Pele utaanza kuagwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Vila Belmiro wa Santos, baada ya shughuli za Luiz Inacio Lula da Silva kuapishwa kuwa Rais wa 39 wa Brazil, leoJumapili.
Pele atazikwa Jumanne, huku shughuli za mazishi ikielezwa zitafanana na zile za Malkia. Uwanja wa Vila Belmiro, unaotumiwa na Santos FC, timu ambayo Pele alitumikia kwa sehemu kubwa ya maisha ya mpira. Uwanja huo ndiyo utatumika kwenye shughuli za mazishi Jumatatu na Jumanne. Santos historia yake haielezewi bila ya kumtaja Pele na ndiyo maana wamelichukua jukumu zima la mazishi yake.
Shughuli za mazishi zitadumu kwa saa 24, kuanzia Jumatatu hadi Jumanne, ambapo jeneza lake litapita mitaani na kupita mbele ya nyumba ya “O Rei’s” mama yake, Celeste. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Brazil, mama yake Pele amelala tu kitandani na anaripotiwa kuwa na miaka 100.