Pele kuzikwa ghorofani

Pele kuzikwa ghorofani

Duuh .. kisa land scarcity or ?
Ndio dear
Hata Israel wanazo sana na hata usa na Japan wao ukitaka ubongo ubaki na mwili uteketezwe unalipa $80,000 in advance

Yaani hata cremation wanaohifadhi zile Urn [emoji3546] watu wanazikimbia wanashindwa kulipia baada ya kuziacha kuchomwa na kuhifadhi sehemu
Dunia hii mpaka unaogopa
 
What happens mwili ukianza kuharibika??
Nafikiri wana njia zao za kuhifadhi ila ninachojua kuna wengine wanazika makaburini halafu baada ya miaka 3 mwili ukisinyaa na kupungua ndio wanahamishia kwenye hilo jengo

Hilo jengo ni tangu 1983 ndio walijenga taratibu wakawa wanaongeza kutokana na demand
Kuna watu wengi sana humo wengine walichomwa pia cremation
 
Yaani we acha tu
Wanaozea humo na wampendwa wanakuja kusalimia kama ziara za makaburini tu

Mimi kuna aina mbili Tatu za kuwaaga wapendwa ndio zimenishangaza

Huko Japan na Arizona [emoji631] kuna watu wametengeneza freezer kubwa za kuhifadhi maiti milele yaani unagandishwa milele na bei yake ni $200,000 wapo waliolipia kabla ya vifo vyao waki secure space

Na huko Tibet hao ndio kiboko maana ardhi yao ni milima na mawe matupu hakuna pa kuzika

Mfalme mmoja miaka mingi iliyopita akataka maiti ziliwe na Ndege waitwao Vultures hao wanakula kila kitu

Kuna watu ndio kazi yao unawapa mpendwa wako nao wanaanza kukata kata na kuwatupia vultures
Ningeweka picha ila sio vizuri

Kama una moyo kaangalie YouTube sky burial ceremony
Usiseme sijatoa onyo
Lol,[emoji3064]
Huyo Pele hivi kwani Brasil hakuna ardhi ya kuzika?
Bora hata hao ambao ardhi yao imejaa mawe.

Watu sasa wanamkufuru Mungu, tuliumbwa kwa udongo na mavumbini lazima tutarudi.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Na kweli sio wamekosa kuzika ardhini hapana bali ni mjini, hakuna sababu za maana
Kweli tunarudi ardhini ila ndio hivyo
 
Yaani we acha tu
Wanaozea humo na wampendwa wanakuja kusalimia kama ziara za makaburini tu

Mimi kuna aina mbili Tatu za kuwaaga wapendwa ndio zimenishangaza

Huko Japan na Arizona [emoji631] kuna watu wametengeneza freezer kubwa za kuhifadhi maiti milele yaani unagandishwa milele na bei yake ni $200,000 wapo waliolipia kabla ya vifo vyao waki secure space

Na huko Tibet hao ndio kiboko maana ardhi yao ni milima na mawe matupu hakuna pa kuzika

Mfalme mmoja miaka mingi iliyopita akataka maiti ziliwe na Ndege waitwao Vultures hao wanakula kila kitu

Kuna watu ndio kazi yao unawapa mpendwa wako nao wanaanza kukata kata na kuwatupia vultures
Ningeweka picha ila sio vizuri

Kama una moyo kaangalie YouTube sky burial ceremony
Usiseme sijatoa onyo
Si bora mara 100 kuchoma? Bado maziko bora ni kuchimbia chini kaburini nyingine zote bado sana.
 
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Brazil, mwili wa Pele utaanza kuagwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Vila Belmiro wa Santos, baada ya shughuli za Luiz Inacio Lula da Silva kuapishwa kuwa Rais wa 39 wa Brazil, leoJumapili.

Pele atazikwa Jumanne, huku shughuli za mazishi ikielezwa zitafanana na zile za Malkia. Uwanja wa Vila Belmiro, unaotumiwa na Santos FC, timu ambayo Pele alitumikia kwa sehemu kubwa ya maisha ya mpira. Uwanja huo ndiyo utatumika kwenye shughuli za mazishi Jumatatu na Jumanne. Santos historia yake haielezewi bila ya kumtaja Pele na ndiyo maana wamelichukua jukumu zima la mazishi yake.

Shughuli za mazishi zitadumu kwa saa 24, kuanzia Jumatatu hadi Jumanne, ambapo jeneza lake litapita mitaani na kupita mbele ya nyumba ya “O Rei’s” mama yake, Celeste. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Brazil, mama yake Pele amelala tu kitandani na anaripotiwa kuwa na miaka 100.
 
Si bora mara 100 kuchoma? Bado maziko bora ni kuchimbia chini kaburini nyingine zote bado sana.
Ni changamoto kwa wasioamini kuchoma
Kama Paris wanazipanga maiti chini kuja juu kwenye kuta ardhini ila tatizo mvua iliharibu basdhi ya makaburi na kulazimu kuyaondoa tena

Tatizo inachukua eneo kubwa la ardhi
Kwa mfano [emoji636] waislam na jews ni lazima wazike na baadhi ya wakristo wasiotaka kuchoma

Sasa mpaka kufikia 2050 itahitajika ukubwa wa NY city kwa ajili ya mazishi tu
 
Nafikiri wana njia zao za kuhifadhi ila ninachojua kuna wengine wanazika makaburini halafu baada ya miaka 3 mwili ukisinyaa na kupungua ndio wanahamishia kwenye hilo jengo

Hilo jengo ni tangu 1983 ndio walijenga taratibu wakawa wanaongeza kutokana na demand
Kuna watu wengi sana humo wengine walichomwa pia cremation
Duhhh
 
Ni changamoto kwa wasioamini kuchoma
Kama Paris wanazipanga maiti chini kuja juu kwenye kuta ardhini ila tatizo mvua iliharibu basdhi ya makaburi na kulazimu kuyaondoa tena

Tatizo inachukua eneo kubwa la ardhi
Kwa mfano [emoji636] waislam na jews ni lazima wazike na baadhi ya wakristo wasiotaka kuchoma

Sasa mpaka kufikia 2050 itahitajika ukubwa wa NY city kwa ajili ya mazishi tu
Asehhh...nashukuru nimejifunza kitu
 
Ukitaka kufikisha ujumbe, jitahidi kuweka maelezo kamili yenye kubeba ujumbe wote...
Ndiyo waandishi wa Mwananchi wa siku hizi, mwingine aliandika nanukuu "...Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani amewakumbusha waendesha pikipiki wote kuvaa element kila wanapokuwa kwenye vyombo hivyo"

Credit kwenu Mwananchi
 
Kuna wale wanaosema Yesu alikuwa Muislam , ila nimefuatilia mazishi ya Yesu ni tofauti kabisa na mazishi ya kiislam. Yesu alizikwa kama kwenye makaburi ya kujengewa lakini wao ilikuwa ni mwamba wameutoboa, akalazwa tuu pale na kuwekewa mlango wa jiwe, HAKUNA CHA MWANANDANI, MWANANJE AU KUKAFINIWA. Na taratibu za kwenda kuupaka mwili mafuta baada ya siku ya tatu kama heshima na mila ya wayahudi. Hao wanaosema Yesu alikuwa mwislam wameyatoa wapi?
 
Lol,[emoji3064]
Huyo Pele hivi kwani Brasil hakuna ardhi ya kuzika?
Bora hata hao ambao ardhi yao imejaa mawe.

Watu sasa wanamkufuru Mungu, tuliumbwa kwa udongo na mavumbini lazima tutarudi.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Kurudi udongoni kupo palepale, ni dhana pana sana,hata huko kwenye jengo kimsingi yupo ardhini tu sababu hata hilo limesimama ardhini,kwa mfano ukiliwa na Fisi kisipatikane cha kuzika itakuwaje?
Fisi akila nyama yako itageuka kinyesi kitarudi kulekule ardhini tu.

Hata usipofukiwa na udongo ukaachwa wazi,funza watakugeuza udongo tu hakuna namna.
 
Kuna wale wanaosema Yesu alikuwa Muislam , ila nimefuatilia mazishi ya Yesu ni tofauti kabisa na mazishi ya kiislam. Yesu alizikwa kama kwenye makaburi ya kujengewa lakini wao ilikuwa ni mwamba wameutoboa, akalazwa tuu pale na kuwekewa mlango wa jiwe, HAKUNA CHA MWANANDANI, MWANANJE AU KUKAFINIWA. Na taratibu za kwenda kuupaka mwili mafuta baada ya siku ya tatu kama heshima na mila ya wayahudi. Hao wanaosema Yesu alikuwa mwislam wameyatoa wapi?
sasa wakienda kuupaka huo mwili mafuta wanaziba pua au? na wanaendelea kuupaka huo mwili hata ukianza kutoa funza? by the way uislamu ulianzishwa na muhamad miaka mingi baada ya yesu kufa
 
Hiyo kauli ya mwisho ndio ipo sawa.
 
Back
Top Bottom