Pema usijapo pema, ukipema si pema tena.
Msemo toka mapema,kiswahili si kibena
Wenye kusema vyema,tungua utaja sema
Ni msemo wa wahenga, wa kufunza ma kurudi
Pema usijapo pema, Utakuja kujutia
Utabakia kuhema,pumzi kujivutia
Ungali ulitetema, ukose kwa luvutia
Pema usojapo pema, ukipema....
Pema usijapo pema, fanya jambo kwa wakati
Uyatende yako mema,ukiweka mikakati
usikubali Neema, ipite wake wakati
Fanya jambo kwa wakati, pema usijapo pema
Sory natumia simu kuandika na ndio makosa mengi na pia sijafanza shairi siku nyingi