Pemba kikombe cha Babu limerudiwa tena

Pemba kikombe cha Babu limerudiwa tena

Haya mambo ndio yanafanya Tanzania iwe kwenye orodha ya nchi zinazoamini ushirikina zaidi duniani.
 
Acha kumfananisha Nyerere na mambo ya ajabu


Katika zama za kupigania uhuru wakati fulani Nyerere aliitwa nyumbani kwa Jumbe Tambaza usiku, nadhani (John Rupia) ndiye aliyetumwa na Wazee kumwita Nyerere, naye akaenda, alipofika akawakuta wazee wakimsubiri, wakamkalisha chini na kumueleza sababu ya yeye kuitwa, akawekwa chini na wakamfanyia dua baada ya dua kuisha likafuata tambiko la mababu, kuliandaliwa Beberu na likachimbwa shimo, beberu likachinjwa huku mchinjaji anachinja kwa kunuia; "Twining amekwisha" wakati huo damu ya beberu ikiachwa ichuruzike mule shimoni baada ya tendo hilo wale wazee wakamuambia Nyerere atambuke lile shimo na huku Wakimwambia: Twining amekwisha nenda zako hakuwezi tenaa!!. Twinning alikuwa ni Gavana wa mwisho wa kiingereza nchi Tanganyika kabla ya uhuru. (Hii ni simulizi ya Nyerere mwenyewe katika moja ya hotuba zake kwa Wazee wa Dar akiwaaga alipong'atuka madarakani).

Katika hotuba hiyo hoyo; anasema alikwenda Bagamoyo kwa Shk Ramia na huko walikesha makaburini wakifanya dua nk.

Hii hotuba ninayo katika moja ya compact cassette zangu na ipo siku nitaiweka humu pindi nitakapotengeneza radio cassete yangu nk.

Je hayo mambo ya kutambuka damu ya beberu na kuomba dua makaburini sio ushirikina??
 
Back
Top Bottom