Thabit Madai
Member
- Oct 8, 2024
- 54
- 140
Naandika andiko hili fupi nikiwa Unguja - Zanzibar baada ya safari ya takribani Wiki Mbili nikiwa kisiwani Pemba.
Mimi ni Mwandishi wa habari na nimepata bahati ya kutembelea maeneo mengi Tanzania bara na Visiwani ila nilichokikuta Pemba bado kinanijastaajabisha hadi sasa naandika andiko hili.
Hivi unaweza kujiuliza kwa karne hii na uchumi tuliokuwa nao kuna Mwanamke anazaa watoto Wanne, Watano na hata Sita huku akiwa hajafika hata miaka 30.
Wacha nikusanue kidogo nilipokuwa Pemba nilitembea mitaani na nilichokigundua kuwa Wanawake wengi hawajui chochote kuhusu uzazi wa mpango, hawajui hata mensturation cycle inafanyaje kazimama mtu mzima hajui tarehe yake ya kuwa hedhini, hajui siku za hatari na salama ni zipi.
Kwa wale wachache ambao wanauelewa kuhusu uzazi wa Mpango na faida zake anakumbana na mitazamo potofu ya watu wanaomzunguka kwamba hana uwelewa wa masuala ya Dini.
Nilipokuwa Pale Wawi ndio nilichoka zaidi nilikutana na Mama ana mimba, amembeba mtoto hajafika hata miaka 2 lakini mkononi anamtoto mwingine ambae kwa kukisia ana miaka Mitatu au Minne.
Nipomhadisia mwenyeji wangu aliniambia mbona ni jambo la kawaida tuu akanieleza kwamba huku unaweza kuona mama na binti yake wanakutana labor.
Anasema kuwa Mama ana mtoto wa miezi mitatu tayari ana mimba kabla hajakaa sawa bint yake ana mimba sasa hapo unakuta mama ananyonyesha na binti yake ananyonyesha.
Mjomba na Mpwa wake wanaumri sawa au Mpwa mkubwa kuliko Mjomba hata ile heshima tena inakuwa haipo tena.
Naiomba Serikali na hataa Mashirika binafsi kuongeza nguvu katika kutoa Elimu ya umuhimu wa Uzazi wa Mpango
Sheria itungwe juu ukomo wa kuzaa
Serikali iangalie kwa jicho la pekee kisiwa cha Pemba na kuongeza kasi ya kukifungua Kisiwa cha Pemba kiuchumi ili watu wawe na shughuli za kufanya na kuacha kuingia mdani mapema na kufyatua Watoto.
Picha kwa Hisani ya Mitandao ya Kijamii, BBC na ripoti juu ya Uzazi wa Mpango