Pemba: Mtoto anayewaka moto akiingia anyanyapawa kwa kuitwa “washawasha”

Pemba: Mtoto anayewaka moto akiingia anyanyapawa kwa kuitwa “washawasha”

G-Mdadisi

Senior Member
Joined
Feb 15, 2018
Posts
165
Reaction score
100
Ukiona mtu mzima analia tambua kabisa kwamba kuna jambo. Faki Hamad Mbarouk mkaazi wa mtaa wa Msigiri uliopo Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba anakabiliwa na mtihani mkubwa ambao umemfanya uso upoteze furaha yake usiku na mchana kutokana na mwanae kukabiliwa na mkasa wa ajabu wa kuwaka moto pindi anapoingia ndani jambo lililopelekea kuchukua jukumu la kulala naye barazani ili kuendelea kumfariji mtoto huyo kwani akiingia ndani nyumba inawaka moto.

UGA TV imefika katika familia ya kijana huyo na kuzungumza na wanafamilia pamoja na majirani juu ya tukio hilo la ajabu ambalo linamkabili mtoto huyo ambapo ameeleza kwamba ikitokea mtoto huyo ameingia ndani nyumba nayo huwa inawaka moto.

Hali hiyo imepelekea uchumi wake kushuka kwani haendi popote katika shughuli zake na badala yake anakaa nyumbani kusubiri kuzima moto.

Mtaani nako mtoto huyo anakabiliwa na unyanyapaa ambapo watu na watoto wenzake wamembadilisha jina na kumuita WASHA WASHA.

VIDEO:
 
Apelekwe kwa wasabato wamuombee atakaa sawa tu
 
Mtoto akiingia ndani tu nyumba inakamata moto na kuanza kuunguza vitu hali iliyopelekea kulazimika kulala nje ili kuzuia hali hiyo.

Zaidi angalia video hapo juu naona wameeleza vizuri wazazi na majirani.
Kuweni creative in a positive way, sio kutunga story za kijinga na kupotezea watu muda, siwezi hata anaglia hiyo video kwanza
 
Sishangai sana wapemba ni wachawi sana tangu jamaa yangu trafic bonge afe hivihivi kama utani wapemba nimewaogopa
 
Hao ni waisiramu mkuu, sasa sabato na uisiramu wapi na wapi kiongoziii
Inabidi wakubali kwa sababu taratibu zao za kidini zimeshindwa kumsaidia huyo mtoto na Hayo ni mambo ya kiimani
 
Back
Top Bottom