Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba linafanya uchunguzi wa vifo vya watu wawili ambao walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Ali Khamis Camp Vitongoji Chake Chake Pemba.
Watu hao ni:
- Othman Hamad Othman miaka 75 mshirazí na mkazi wa Kimango-Kiungoni Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
- Amour Salim Khamis miaka 28 mshirazí na mkazi wa Kimango-Kiungoni Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Uchunguzi huo unaendelea kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali pamoja na walioshuhudia ukamatwaji wa watu hao.