Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
- Thread starter
- #21
Kwa Pemba hakuna dogo! Ingekuwa kama Rorya ambapo Pinda alipropose kupeleka jeshi, ingekuwaje?
SIo hakuna dogo ,yaliotokea Pemba ni mambo ambayo yamewacha historia ,huko Tarime na Rorya ni wananchi against wananchi ,ndiko kunakofaa kupelekwa jeshi ,polisi au FFU lakini sio Pemba ,vyombo hivyo vikipekwa huko Pemba kwa wingi huo vinahesabika vinakwenda kufanya machafu ,kuwadhalilisha watu, inaeleweka CCM walijitangazia ushindi sasa ilikuwaje kuwaje watu kuuliwa na kuingiliwa majumbani ? Kufikia vyombo hivi kufanya machafu katika sehemu moja ya nchi yao ujue kuwa sehemu hiyo automatic itajihesabu sio sehemu ya Nchi na kwa hivyo Pemba wamejihesabu kuwa wao si WaTanzania na sababu hiyo ndio moja kati ya sababu zinazopelekea wao kuwa na madai UN.
Hapa nataka upime sana usiwe mbishi wala usiwe na jazba kwa kuwa wewe tu ni mpenzi wa CCM au ni Mtanganyika , chukulia linatoka jeshi na mapolisi wanavamia Kigoma na kutenda udhalilishaji wa kuingilia mwanafamilia mbele ya familia ,mke mbele ya mumewe na watoto wake ,wanapiga wanalawiti na kufanya kila ovu unalolijua wewe(Pemba yamefanywa hayo na hao mnaowaita waliokwenda kwenye au waliomo ndani ya nchi yao).
Sasa wamefanya uasherati huo hapa Kigoma ,hivi wananchi wa Kigoma watahisi vipi ? Polisi na majeshi wamekwenda kufanya unyama ndani ya nchi yao tena baada ya Chama wanachokiunga mkono kujitangazia ushindi ? Chombo cha dola kinafanya mambo ya udhalilishaji ndani ya nchi inayojitawala tena kidemokrasia halafu Raisi wa Nchi anarudi kuwapachika vyeo ? Wewe kama una akili timamu pima na utoe jibu ? Kama unafurahia sio mbaya kila mtu anaujua uzima wa akili yake kwa vile anvyojiona yeye ni mzima. Kwa mimi nitakuona ni taahira japo mwenyewe unajiona mzima.
Hivyo unaposema hakuna dogo basi ujue kuwa yaliopita Pemba si mambo ya kuonekana kuwa ni madogo ,ni unyanyasi mkubwa ambao umefanywa na apitae kufanya unyanyasaji huo(Ubakaji) hufananishwa na mnyama na Kikwete analifahamu hilo kutokana na dini yake au yetu.
Je tunatawaliwa na wanyama ? Hivyo kama kuuliwa wapemba wameshauliwa,kama kunyanyaswa wameshanyanyswa kama kunajisiwa wameshanajisiwa sasa wanataka nini zaidi au wanaogopa nini zaidi huoni kama wapo tayari hao waliobakia nao kufa ,watakaokimbia watakimbia na watakao kufa na mtu watakufa lakini hakuogopwi tena ,lolote litakalotomezwa basi lijue kuwa huko linakotomezwa vilevile kifo kipo.Lakini mambo ya kuvumiliana yameshafika mwisho kwa Pemba sasa huko Tarime na Rorya kama bado ni huko na sio Pemba ya kwenu bado ni madogo.