Penati Ilivyoota Mbawa

Kukosa penati hiyo kuliwatoa wachezaji mchezoni huku mashabiki wakinyong'onyea maana walishindwa kuamini aliyepiga ni Samatta au Abdi Kassim (Barrack wa Unguja aliyekuwa anapiga penati Kizenji)!
kuna upigaji ambao unaendelea kujiuliza maswali mengi sana ....nakumbuka Yanga wameshatimua wapigaji wengi wazembe akiwemo Jobe Ayubu 'Kwasakwasa' na hivi karibuni simba walimtimua Mussa Mude ingawa kwa simba sishangai maana hata red card wanakutimua
 
Mlitaka muifunge Misr, toka lini?
Tulitaka tuifunge Misri toka siku hiyo. Haiwezekani sie tuendelee kuwa kichwa cha mwendawazimu. Sasa tunaelekeza nguvu kwa Nigeria kusaka heshima tu maana hatuwezi kufuzu hata kama wachawi wote wa Tanzania wataunganisha matunguri yao kwa pamoja.
 
ndugu yangu tutakuwa na uwezo wa kujipanga na kuifunga Misr pale ligi yetu itakapoachanishwa na siasa. CCM kwa vile ndo mmiliki wa viwanja vya michezo nchini haiko tayari kuona simba na yanga zinashuka daraja kwa sababu ndo mtaji wake.

Na viwanja ni vibovu kwelikweli
 
Samata ameshakishwa yule, Atafute totto la kizungu amjaze apate visa ya kuish Europe
Tanzania tuna safari ndefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…