Pendekeza Majina ya Wabunge wapya ambao ungependa waingie Bungeni Hapo Mwakani

Pendekeza Majina ya Wabunge wapya ambao ungependa waingie Bungeni Hapo Mwakani

Ndugu zangu watanzania,

Sauti ya wengi ni Sauti ya Mungu. Maneno huumba. kwa kuwa mwakani ni Mwaka wa uchaguzi ,na kwa kuwa kuna wabunge wengine walishatangaza kustaafu siasa na kwa kuwa kuna wabunge wengine kutokana na Umri wanaweza kustaafu ubunge na kwa kuwa wengine kutokana na sababu mbalimbali wanaweza wasitake kugombea tena.

Na kwa kuwa uongozi ni kupokezana vijiti na kwa kuwa ubunge ni utumishi wa watu unaohitaji mtu kujitoa na kujitolea kwa ajili ya watu na kutambua kuwa uongozi ni utumishi kwa watu na kwa kuwa CCM ndio chama kinachoaminika katika mioyo ya watanzania na kupendwa na watanzania na hivyo kuwa na imani kubwa na wagombea kupitia CCM.

Je watanzania wenzangu mlikuwa mnatamani sura zipi Ngeni ambazo hazipo kwa sasa bungeni kuona zikipata nafasi ya kuingia Bungeni kupitia majimbo kwa chama cha Mapinduzi? Mnatamani nani na nani kuwaona Bungeni?

Kwa upande wangu japo nataja wachache lakini haimaanishi ni hao hao.wapo wengine ambao nitawataja baadaye.leo nataja tu lakini sababu nitaeleza baadaye.

.Mheshimiwa Paul Makonda.RC Arusha.

. Mheshimiwa Amos Makala.Mwenezi CCM Taifa.

. Mheshimiwa Nehemiah Mchechu,msajili wa Hazina.

. Mheshimiwa Jokate Mwegelo.Katibu Mkuu UVCCM

. Mheshimiwa David Kafulila.Mkurugenzi PPP.

. Mheshimiwa Juma Homela.RC Mbeya.

. Mheshimiwa Shaka Hamidu Shaka.Dc huko Morogoro

. Mheshimiwa Gerson Msigwa.Katibu Mkuu wizara ya utamaduni,sanaa na Michezo.

Muda huu naishia hapa ila nitaendelea wakati mwingine kuwapa sababu ya kupendekeza jina la kila mmoja hapo juu na kuongeza baadhi ya majina mengine mapya. Sijataja majimbo maana mtu anaweza kugombea jimbo lolote lile.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wanasiasa mwogopeni Mungu,
Imeandikwa kwenye kitabu gani kuwa "sauti ya wengi ni sauti ya Mungu"
Kipindi cha Nabii Nuhu kulikuwa na sauti za watu wagapi wakipinga Nuhu na Safina yake?
Je waliookolewa walikuwa wengi au kidogo?
Vipi kipindi cha Mtumishi wa Mungu Lutu waliookolewa na ule moto wa Sodoma na Gomora wengi au wachache walio kuwa watiifu?
 
1.Mh Godbless lema
2.Mh Dr Wilbroad Slaaa
3. Mh Sugu
4. Mh John Heche
5. Mh Mch. Msigwa
 
1.Mh Godbless lema
2.Mh Dr Wilbroad Slaaa
3. Mh Sugu
4. Mh John Heche
5. Mh Mch. Msigwa
Hawa ni wasaka Tonge na wachumia tumbo tu. Hawana lolote wanaloweza kusaidia katika mawazo chanya ya ujenzi wa Taifa letu.kwa sababu ni watu wa Ndimi mbili.
 
Hawa ni wasaka Tonge na wachumia tumbo tu. Hawana lolote wanaloweza kusaidia katika mawazo chanya ya ujenzi wa Taifa letu.kwa sababu ni watu wa Ndimi mbili.

Hawa ni wasaka Tonge na wachumia tumbo tu. Hawana lolote wanaloweza kusaidia katika mawazo chanya ya ujenzi wa Taifa letu.kwa sababu ni watu wa Ndimi mbili.
Mkuuu rekebisha kichwa cha huu uzi basi,,, au weka masharti kwamba wachangie wana sisiemu tu,,,
Maana mawazo yangu na mapenzi yangu huyataki,,,
Acha u****e.😎
 
Utaishia kupigishwa magoti A$$ L!CKE®
20240823_211619.jpg
 
Kumwacha nje Luhaga Mpina kunaonyesha hauko serious.
Au unatafuta wabunge wa 'ndiyo mzee' peke yake?
 
Hivi Lucas Mwashambwa akili yako iko sawa kweli?
 
Ni basi tu watu hawana uelewa na mambo katika watu hawana kazi hapa Tanzania ni Wabunge.
Wanakula pesa za walipa kodi bure tu.
 
Hebu siku moja moja karibu kiwa serious tumechoka na vichekesho vyako.
 
Back
Top Bottom