Pendekezo: Barabara ya Kimara-Kibaha iitwe Magufuli Highway

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Ili kumuenzi hayati John Magufuli kwa kazi zake nzuri za ujenzi, Kipande cha Barabara ya Kimara hadi Kibaha kibadilishwe jina kutoka morogoro road na kiitwe MAGUFULI HIGHWAY.

Hii itaacha kumbukumbu kwa vizazi vijavyo ma pia itaonyesha kudhamini mchango wake hasa kwenye ujenzi wa miundo Mbinu.

Tunaomba rais pamoja na baraza lako ulifikirie hilo.
 
KIBAHA-MOROGORO tuiite JINA GANI MKUU? Mie nadhani tusubiri Hiyo HIGHWAY ikifike Mwisho ndio tutafute jina inawezekana ikaitwa JINA LAKO MUNGU sio ATHUMANI
 
Hatujawahi kuwa na Rais mchapakazi namna ile, anayeshinda site na kuipitia hata ile miradi tuliyoidharau na kuiona midogo, hilo moja ni la kuenziwa na nitamkumbuka kwalo!
Kwani si naskia huko aliko pamoja na kuwa kiongozi mkubwa, kuna mabarabara na mitaa imepewa kwa jina lake sasa tatizo nini tena?
 
Kwani si naskia huko aliko, pamoja na kuwa kiongozi mkubwa, kuna mabarabara na mitaa imepewa kwa jina lake sasa tatizo nini tena?
 
Ukiona mvua inayotengenezwa walowesha hata japo kibanda cha kujikinga hakuna; inatia huruma sana hii barabara.
 
Unataka kuleta laana barabarani ili kila dk magari yawe yanapinduka ?
 
Serikali iwalipe fidia wahanga walioshinda kesi mahakamani Kwa kubomolewa nyumba zao bila kulipwa fidia na Marehemu gaidi Jiwe kupisha ujenzi wa hiyo barabara. Huyo Marehemu gaidi barabara ya airport Ilemela to Mwanza mjini ndio iitwe Jina lake
 
Hii barabara aliijenga kwa lawama nyingi sana, inashangaza wameshindwa hata kuifikisha Chalinze na kimsingi ilitakiwa igote hapo
 
Kibaha -morogoro itabaki kuwa Morogoro Road au Morogoro Highway
Basi hata hii ya Kimara -Kibaha ibaki Morogoro Highway mbona MAGUFULI alikataa Daraja la Kigamboni kuitwa JAKAYA KIKWETE na ndiye Aliyelijenga?
 
Mipango miji mibovuu inapelekea hata miradi mikubwa kama hii haivutii inavyostahili barabara imepindapinda kama nyoka..
Tunawatendaji uwezo wao ni wa chini sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…