Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kufuatia taarifa iliyotolewa rasmi leo (pia kuletwa humu JF) kuhusu kushindwa kufanyika kwa vikao vya bunge la Afrika mashariki (EALA) kwa sababu za ukata uliotokana na baadhi ya nchi wanachama kushindwa kuleta michango yake kwa wakati, nimetafakari na kuwaza kwa kina ilo kuona tija na mantiki ya kuwepo kwa bunge hilo na kugundua kwa 100% hakuna!
Hapa ni baadhi tu ya hoja za kuonyesha namna chombo hicho kinapaswa kufutwa, tena haraka sana.
1. Kila nchi mwanachama (pasipo kuzingatia ukubwa wa kieneo, idadi ya watu na nguvu za kiuchumi) ina nafasi sawa ya kupeleka wabunge wake 9. Nini magic ya kuwa na wawakilishi 9 kwa kila nchi?
2. Ni bunge lisilokuwa na meno yoyote ya kusimamia utendaji wa nchi yoyote ile mwanchama katika ukanda huu. Mfano mzuri ni mzozo wa sasa wa DRC na M23.
3. Wabunge wa hilo bunge hupatikana kupitia migongo ya vyama vya siasa vya nchi wanachama. Kwa Tanzania maana yake ni wapambe wa CCM ndio wamejaa kule.
4. Uendeshaji wa shughuli zake unahitaji bajeti kubwa ambayo baadhi ya nchi wanachama hawawezi kuzibeba. (Yaani kwa umaskini uliokithiri South Sudan na Burundi, ni mzigo mkubwa mnoo kuwaambia wachangie uendeshaji wa hilo bunge). Na kukosekana kwa pesa kunapelekea hilo bunge kushindwa kushughuli zake.
5. Uamuzi wowote wa bunge hilo hauwezi kutekelezwa popote ndani ya hiyo jumuiya mpaka usubiri kamisheni ya wakuu wa nchi wanachama wairidhie. Na kamisheni ya wakuu wa nchi wakiikataa au hata nchi moja ikikataa, basi huo uamuzi utakuwa umekufa kifo cha mende. Hivyo maamuzi ya hilo bunge yanabakia kuwa ni ushauri tu kwa nchi wanachama na sio sheria.
6. Maamuzi yoyote ya wakuu wa nchi katika vikao vyao, hayasubiri wala hayafungwi na uwepo au kutokuwepo kwa hilo bunge la Afrika mashariki.
Ikiwa kuwepo kwa hilo bunge zaidi ya miaka 20 hakuna matunda yoyote tuliyopata zaidi ya kodi zetu kutumika kuwanufaisha wengine, ni wakati sasa kufutwa haraka sana kwa hilo bunge ili kubakia na Kamisheni ya wakuu wa nchi tu.