kipenseli2021
JF-Expert Member
- Jul 17, 2021
- 1,390
- 1,431
UTANGULIZI
TEHAMA au Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni mkusanyiko wa watu,vifaa vya kompyuta na mawasiliano,programu na data ambazo zinachakatwa na kutoa au kupata taarifa zinazo tumika katika nyanja mbalimbali.
Maendeleo ya TEHAMA katika nchi yetu na Dunia yanazidi kuongezeka kwa sababu ya mahitaji makubwa ya taarifa kutoka katika Data zilizo changatwa ili kuzidi kuchochechea maendeleo ya sekta mbalimbali mfano sekta ya elimu,kilimo,biashara na uchumi,utamaduni,utalii na sekta nyingine.
Kiungo au vitu muhimu katika TEHAMA ni watu(user), vifaa vya mawasiliano(hardware),programu(software),mtandao (network) ,data na taarifa(information)
hivyo maendeleo ya TEHAMA yanazingatia kuendeleza moja katika ya sehemu nilizo zitaja ambazo zinaunda TEHAMA(Teknolojia ya Habari na mawasiliano) mfano kuboresha vifaa na usambazaji wa data
FAIDA YA TEHAMA
Teknolojia ya Habari na mawasiliano ina faida nyingi sana katika kila sekta kubwa kabisa ikiwe ni kuongeza thamani ya huduma na bidhaa katika sekta au kwa ufupi ni kuleta faida katika biashara(BUSINESS VALUES AND PROFIT)
Faida nyingine za TEHAMA(Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) ni kama zifuatazo
MAPENDEKEZO
Kwa kuzingatia umuhimu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na nikizingatia kuwa kuna kundi kubwa la watu ambao ni zaidi ya asilimia 20 wanaoishi vijijini kwa mujibu wa takwimu ambao wameachwa kwenye giza la matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano.
hivyo nashauri serikali ianzishe Chombo/wakala ambaye atahusika na kusimamia au kuchochea Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasilino ambaye tukiite WAKALA WA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO VIJIJINI,pia wakala huyu aende sambamba na REA na TARURA ili kuweza kusaidia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
PENDEKKEZO: Majukumu ya msingi ya WAKALA WA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO VIJIJINI
FAIDA AU MATOKEO YA KUANZISHWA KWA WAKALA WA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO VIJIJINI
JE, KUNA UMUHIMU WOWOTE WA WAKALA HUYU
Jibu ndio,watu wanao ishi vijiji ikiwemo watendaji wa serikali wanaingia gharama kubwa sana wanapo taka huduma ambazo zinapatika kwenye mtandao mfano huduma za uhakiki wa vyeti vya Kuzaliwa (Uhakiki RITA),uandikishaji wa biashara (BRELA),Uombaji wa mikopo ya chuo kikuu (HELSB),uombaji wa vyuo kwa ngazi mbalimbali ,uombaji wa ajira (AJIRA PORTA) na huduma mbalimbali ambazo mtu wa kawaida kabisa alitakiwa aweze kufanya mwenyewe kwa gharama ya BANDO chini ya elfu moja.
Pia ingesaidia kuwaongeza matumizi au upatikaji wa HUDUMA ZA SERIKALI hili kuzidi kupungu foreni na gharama
HITIMISHO
Napendekeza serikali isiwaache watu wa vijiji nyuma kwenye maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hivyo ianzishe wakala huyu aweze kusaidia kuleta maendeleo ya Teknolojia ya Habari na mawasiliano na kuwatoa watu wa vijiji gizani kwa FIKRA.
Imeandaliwa na Kipenseli aka Mpenda haki

- kurahisiha mawasiliano au kubadilishana kwa taarifa
- kuongeza uwazi na uwajibikaji katika Serikali na Taasisi zake
- kurahisha na kuongeza soko la bidhaa na huduma (E-business and E-commerce)
- kusaidia kujifunza kwa njia ya mtandao (E-learning)
- kusaidia utoaji wa huduma za serikali (E-goverment)
MAPENDEKEZO
Kwa kuzingatia umuhimu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na nikizingatia kuwa kuna kundi kubwa la watu ambao ni zaidi ya asilimia 20 wanaoishi vijijini kwa mujibu wa takwimu ambao wameachwa kwenye giza la matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano.
hivyo nashauri serikali ianzishe Chombo/wakala ambaye atahusika na kusimamia au kuchochea Maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasilino ambaye tukiite WAKALA WA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO VIJIJINI,pia wakala huyu aende sambamba na REA na TARURA ili kuweza kusaidia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
PENDEKKEZO: Majukumu ya msingi ya WAKALA WA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO VIJIJINI
- Kusimamia na kuimarisha miundi mbinu wezeshe ya teknolojia ya habari na mawasiliano vijijini
- Kusimamia na kuimarisha miundo mbinu ya TEHAMA katika shule,vituo vya afya,vituo vya polisi,serikali za mitaa ili waweze kuweka na kutumia TEHAMA
- Kuwa na ma afisa watakao kuwa wanatoa huduma na elimu hitaji ya TEHAMA kama Huduma za serikali mtandao
FAIDA AU MATOKEO YA KUANZISHWA KWA WAKALA WA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO VIJIJINI
- Kuunganisha vituo vya afya vilivyopo vijijini na vituo vikubwa vya afya kama Muhimbili,Benjamini Mkapa,KCMC na hospitali nyingine
- kuunganisha vituo vya kutoa huduma mfano TRA na makao makuu hivyo itasaidia ulipaji wa kodi zaidi
- kuwezesha shule za msingi na sekondari kuweza kutumia TEHAMA kwa ajili ya kujifunza,kupakua vitabu na elimu mtandaoni
- kumuwezesha mkulima kupata bei halisi ya bidhaa au mazao ivyo ataweza kukadiria bei sababu anajua bei halisi ya kwenye soko
- kuwawezesha kupata taarifa za hali ya hewa au mabadiliko ya hali ya hewa

Upvote
3