Pendekezo: Jangwani paboreshwe Wamachinga wa Kariakoo wahamishiwe hapo

Feki hapana aisee niambie ni less-quality ambao huletwa kulingana na hali za kiuchumi za wananchi zilivyo.
Mkuu 'Joselela,' sasa naona tatizo lako lilipo. Hujui maana ya "vitu feki" ni nini.

Hiyo uliyoipachika jina la "less-quality", ni kitu gani hicho? Soko haliwezi kuwa na vitu vya aina hiyo; kwamba pawepo na vitu vinavyotengenezwa kwa makundi maalum vyenye ubora tofauti.

Ni lazima pawepo na viwango vinavyofuatwa kwa kila bidhaa inayouzwa sokoni bila ya kubagua ni watu gani wanastahili kuvinunua.
 
'Definition' isiyochanganya mtu yeyote kuhusu hayo unayoyasema hapa ni rahisi.

Chukulia viatu vinavyotengenezwa na kampuni mashuhuri ya Nike.

Nike anatengeneza viatu vya aina mbalimbali na vyenye bei tofauti kutokana na sababu mbalimbali za utengenezaji wa viatu hivyo.

Inapotokea mtu au kampuni nyingine, kwa mfano toka China, wakaigiza utengenezaji wa viatu hivyo vya mfanano kwa kila kitu, hata kama ubora wake ni uleule, au hata zaidi, halafu akaleta vitu hivyo na kuvimwaga sokoni, kana kwamba vimetengenezwa na Nike. Viatu hivyo ni 'Feki.'

Hali ni hiyo hiyo hata kwenye madawa na vitu vingi vingine.

Kitu muhimu zaidi kwa walaji (wanunuzi) ni kukosekana kwa uthibitisho wa ubora wa vitu hivyo na taasisi zinazotakiwa kuthibitisha. Vitu hivyo vinakosa uthibitisho, kwa sababu ni vya 'wizi', vinatengenezwa bila idhini ya mwenye miliki wa kutengeneza vitu hivyo.

Serikali kamwe haiwezi kuruhusu hali ya namna hiyo iendelee ndani ya nchi yoyote kwa sababu mbalimbali.
 
Umachinga hauwezi kuisha maana hata dunia ya kwanza wametengewa maeneo yao. Dawa ni kutenga maeneo vijengwe vibanda designed kwa kuchukua nafasi ndogo halafu wapewe kwa bei rahisi hata kama watalipa elfu 30 kwa mwezi.
 
Unahitaji serikali ya miundo mbinu, siyo serikali ya pesa nyepesi mikononi mwa watu.
 
Hapana pale panajaa maji wawapeleke kawe Tanganyika Packers pana eneo kubwa la uwanja ni pazuri vipindi vyote watafanya kazi
 
Hapana pale panajaa maji wawapeleke kawe Tanganyika Packers pana eneo kubwa la uwanja ni pazuri vipindi vyote watafanya kazi
Mwamposa atatangaza mfungo wa kupinga hili
 
Tatizo la machinga ni uthibitisho wa ubovu wa elimu yetu na mifumo hewa ya kuwaandaa vijana (youth incubation)!
Kuwahamishia sehemu fulani wala si suluhisho.

Nadhani ipo haja ya baraza la mawaziri na bunge kuja na mpango mkakati wa makusudi kwa hati ya dharura ili kutoa suluhisho!

Najua wewe unamaanisha wale machinga wauza mitumba. Kwa taarifa yako kuna mfumuko wa machinga machangu na bodaboda. Kwenye hiyo listi ongezea vijana wa UVCCM wale waviziaji wa teuzi!
 
Watu kama hawa Nyerere aliwapeleka Gezaulole wakalime.
Siyo kuwapa maeneo ya wazi ili wayachafue. Ni wengi na wataongezeka kila kukicha kila mji!
Yule aiyekuwa waziri wa elimu Mulugo amesema vijana milioni 1.8 wanamakiza shule za msingi next year. Unataka waje jangwani pia?
Tena hili siyo tatizo linaloweza kutatuliwa na team za ma RC na DC tunaoletewa. Wazecha- karata! ( Opportunists)

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwa sasa mambo ya ujamaa kuwapeleka watu mashambani haifai tena. Hawa watu wana umuhimu wao katika mazingira tuliyonayo.

Pia kwa sasa inatakiwa suluhisho kwa tatizo lililopo wakati inatafutwa solution ya muda mrefu.
 
Mkuu kwa sasa mambo ya ujamaa kuwapeleka watu mashambani haifai tena. Hawa watu wana umuhimu wao katika mazingira tuliyonayo.

Pia kwa sasa inatakiwa suluhisho kwa tatizo lililopo wakati inatafutwa solution ya muda mrefu.
Wapelekwe machinga complex kariakoo bei zishushwe
 
Hapana pale panajaa maji wawapeleke kawe Tanganyika Packers pana eneo kubwa la uwanja ni pazuri vipindi vyote watafanya kazi
Pale kawe pia panaweza kutumika na panafikika kirahisi. Ninakuunga mkono ili hapo pia paboreshwe kwa kujengwa modern booths ili hawa ndugu zetu pia waendelee kujikimu kimaisha.

Hayo maeneo mawili ya jangwani na tanganyika packers yanaweza kusaidia sana kupunguza wamachinga kwenye barabara.
 
Pia pawepo na stand ya mabasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…