Mwelekeo wa hali ya uchaguzi unasikitisha kidogo. Matukio ya vurugu za hapa na pale unanifanya nitamani kuwa wagombea wa Urais wa kianzia na Kikwete wakutane ili kulipa taifa picha ya umoja katika tofauti. Watoe kauli ya pamoja ya kuwakata wanachama wao na mashabiki kutotumia nguvu na wale wenye vikundi vya ulinzi wawatulize makada wao. Vinginevyo, tujiandae kulipa gharama kubwa zaidi. Wafanye mapema
Mzee Mwanakijiji, asante kwa ushauri huu, ni ushauri wa busara unaohitaji wenye busara za kihivyo kuufuata, very unfortunately, rais wetu, Mheshimiwa sana, Jakaya Mrisho Kikwete, sio mtu mwenye busara kihivyo. Please correct me if I'm wrong, hivi kama rais wako sio mtu mwenye busara, jee kusema rais Kikwete hana busara za kihivyo itakuwa ni kumkosea adabu?. Naamini sio, haswa kama nitathibitisha kutokuwa na busara kwake kwa
baadhi ya kauli zake, zilizohitaji kiwango cha busara za wastani tuu ambazo nazo hanazo.
Jinsi alivyoshugulikia lile tishio la mgomo wa wafanyakazi kwa lugha ya vitisho, kebehi, dharau, bezo, mapuuza, kiburi na jeuri isiyo kifani ndio kipimo cha busara za JK. Kama anaikimbia midahalo tuu ya kuonyesha uwezo wake mbele ya washindani wake, leo atakuwa na audacity ya kukutani na washindani wake kuitakia mema nchi hii?!. Mwenzio
anawaza utawapa mtaji wa kisiasa.
Naamini kuna wenye busara wengi tuu CCM na serikali ambao huwa wanamshauri rais wetu nini cha kufanya/sema wakati gani, lakini anawapuuza, kwa kifupi rais wetu hashauriki, he is too proud to bow down to the people for the sake of this nation. Hizo picha mnazoziona mpaka anakaa kwenye mavumbi ni pure pretence, pride inaonekana wazi kwenye paji la uso wake, ana bend down ili aonekane down to earth kuombea kura!.
Tatizo jingine kubwa la rais wetu huyu JK linalofanya kutokubali kuutekeleza ushauri kama huu ni dharau na mapuuza almost kwenye kila kitu, he is never serious on serious maters na kikubwa zaidi hana hata chembe ya aibu when he does mistakes as if yeye ni malaika.
Wakati wa ule mkutano wa CPA wa Arusha, JK alikuwa aufungue saa 3:00 asubuhi, mheshimiwa sana alifika saa 5:17!, just imagine kuwangojesha wageni wote hao tena wa kimataifa kwa muda wote huo, tena afadhali yetu sisi waswahili, wazungu wale waligeuka wekundu. Haya hatimaye alifika na kuufungua, for whataver the reasons zilizopelekea kuchelewa, he had an obligation just to say sorry na kutoa sababu yoyote, un avoidable circumstances zilizomfanya achelewe, he said nothing!, alifika akaufungua as if nothing happened na hiyo saa 5 ndio ilikuwa schedule yake. Wastaarabu huwa wanasema japo sorry to keep you waiting, yeye wala!, huyu ndio leo akae na wenzie kwa pamoja wahubiri amani?!, not this JK, na baada ya uchaguzi sikilizieni hayo mabezo yatakayofuatia.
JK ni rais wetu, heshima yake kama rais iko pale pale, lakini kueleza madhaifu yake, isichukuliwe kama ni kuvunjia heshima kwa wenye busara, huku ni kumjenga.