Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Huu ndio wakati wa kuanza kutumia lugha ya Kiswahili kufundishia katika ngazi zote za elimu nchini
Pamoja na Kiswahili kupitishwa na Sera ya elimu mwaka 2014 bado hakijaanza kutumika kufundishia masomo katika elimu ya upili na elimu ya juu.
Sera ya Elimu ya mwaka 2014 inasema Kiswahili pamoja na kingereza zitakuwa ni lugha za kufundishia kuanzia elimu ya awali hadi elimu ya juu, lakini takribani miaka 6 imepita bila suala hilo kutekelezwa.
Tafiti nyingi zilizofanywa zilionesha kuwa lugha ambayo unaweza kuwapa maarifa na kuwafanya wanafunzi kuwa wavumbuzi ni kiswahili (rejea utafiti wa Mzee Makweta) licha ya tafiti kuonesha kuwa Kiswahili kilifaa kutumika kufundishia bado wadau wamekuwa wakilegalega kutoa maamuzi.
Mwaka 1991 ilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuanza kufundishia masomo yote kwa Kiswahili lakini ilishindikana kutokana na ugumu wa kufanya maamuzi badala yake wakaishia kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano rasmi chuoni hapo.
Wapo baadhi ya watu pamoja na wataalam wengine wasio fuatilia mambo na kufanya uchunguzi wanaobeba madai yasiyokuwa ya kweli kuwa hakuna vitabu!
Mwaka 1972 vitabu vya Kemia na Baiolojia vya Lambert na Habort vilitafsiriwa na kuwa kwa Kiswahili kama mataifa mengine ya ulaya yalivyotafsiri vitabu hivi kuwa katika lugha zao.
Pamoja na hayo kwa sasa kuna vitabu vya Kiswahili vya sekondari vya Historia, Biolojia, kemia, fizikia, Geografia nk. Vilivyoandikwa kwa kiswahili.
Kiswahili kinavyoweza kutumika kufundishia masomo yote
Kiswahili kinaweza kuwa lugha ya kupitishia maarifa huku lugha ya Kingereza na lugha nyinginezo zifundishwe kama kozi ya lazima kuanzia awali hadi vyuo vikuu kuliko kingereza cha sasa kinachofundishwa kama somo na kutofuata kanuni zozote za ufundishaji lugha ya kigeni.
MKAZO
Hakuna nchi yeyote yenye maendeleo ya kweli kwa kutumika lugha ya watu wengine, kwasababu lugha ni uchumi Na ukitaka kukuza lugha yako lazima ukuze uchumi na hatimaye lugha hukuza uchumi.
Mkosi ulipoanzia, kama asemavyo profesa Mbaabu (2007), kuchapishwa kwa Kitabu cha African Education (1953) pamoja na mkutano wa elimu ya kiafrika 1953, mkutano ambao uliripoti kuwa kuchapishwa kwa African education ni hatua mkubwa katika mabadiliko ya sera ya uingereza kuhusu elimu ya Africa hasa afrika mashariki.
Kitabu hicho kilipendekeza kwamba, kusomeshwa kwa kiswahili kukomeshwe kwa sababu ndicho kizuizi kikubwa dhidi ya maendeleo ya kingereza. Serikali ya uingereza ilikuwa tayari kuanzisha mabadiliko yeyote ambayo yangesaidia kukabiliana na mwamko wa uzalendo wa Mwafrika ambao uliyatishia mamlaka ya kikoloni kwa kupigania uhuru.
Kuondolewa kwa kiswahili kungepunguza uwezekano wa mawasiliano kati ya makabila na kungesaisia kuua mwamko na mtazami wa kitaifa kati ya RAIA.
Jambo hilo lingehakikisha kwamba uingereza ingeendelea kuathiri nchi hizo hata baada ya uhuru ( Mbaabu I.(2007) Historia ya usanifishaji wa kiswahili)
Hitimisho
Ni wakati sasa wa kuahamisha maarifa yaliyomo katika lugha nyingine na kuyahamisha katika lugha ya Kiswahili na kisha kujifunza maarifa hayo kwa lugha yetu kama walivyofanya kisumeri kwenda kiakadi 2350kk, na Kigiriki kwenda Kiingereza- Kijerumani-Kfaransa nk.