Achana na China haiwezi kukusaidi kitu, ongelea Taifa lako.
China wamekataa cheo cha kuwa developed ili wapate 'fursa' fulani za kiuchumi. Kwa ulingano ni kwamba vyuo vinavyofundisha kwa kichina ni vingi kuliko kiingereza.
Ishu za kilatini ni misamiati na inatoholewa kwenda kwenye lugha mbali mbali ili kurahisisha uelewa.
Unajua hata kiingereza huwa tunasema kuna watu wanaongea kiingereza kigumu na ugumu wenyewe ni maneno tu ambayo hatuyajui na hayatumiki mara kwa mara.
Ni kweli hii lugha hatuielewi pamoja na kwamba ndio inayotumika kufundishia wakati huu hivyo hizo faida za kiingereza tunazikosa vilevile.Wengi wa binadamu wanaopigia chapuo huu mswada mfu watoto wao wamewapeleka English Medium Schools, hawataki kuwa mfano. Kiingereza ni lugha kubwa, kujifanya tunapenda saana Kiswahili ni kichaka cha kuficha kushindwa kwetu kumudu Kiingereza.
Wachina walianza kuendeleza teknolojia ndogo ndogo za mashambani ndio wakajifungia. Sisi tunaanza na mdomo
Sasa hapo ndio pa kujiuliza inakuaje hivyo wakati sasa tunatumia kiingereza kufundishia? Kama kufundishwa kwa kiingereza ndio kunafanya tujue kiingereza sasa mbona wabongo hatujui hicho kiingereza hadi hao wenye PHD bado pia kiingereza kinawapa tabu?Yaani kwa kuwa jamaa lugha inamgonga ndiyo unaleta pendekezo hilo sasa, hapana. Mtu ni PhD holder halafu simple english inamtoa kamasi inaahangaza .
Kwani mbona hata sasa wakenya wanatuburuza sana tu kwa kuwa sie hatujui hicho kiingereza?Siku makampuni yatakapokuwa yanaajiri watu wa nje kwa sababu wa ndani hawajui english msianze kulialia...
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio tujifunze sasa, kwani hakuna muujiza. Tuna tabia ya uzembe, kitu kikitushinda tunakiharamisha. Kwani yale tunayojifunza kwa Kiswahili hatufeli?Kwani mbona hata sasa wakenya wanatuburuza sana tu kwa kuwa sie hatujui hicho kiingereza?
Kumbe watu wanapeleka watoto zao hizo shule ili tu wajue kiingereza na si kwamba wanawapeleka kwa ubora wa elimu! Ndiyo maana kuna baadhi ya watoto unakuta anaongea kiingereza vizuri tu ila kichwani hakuna kitu.Wale wanaotamani Kiswahili iwe lugha yakufundishia mashuleni hawapeleki watoto wao kwenye hizo shule za kiswahili wanawahangaikia kuwapeleka kwenye shule za English Medium.Haiwezekani ukapuuza lugha ya Ulimwengu kingeleza yaani English ukakazania lugha inayotumika katika nchi yako tu.Hata kama kiswahili kinatumika nchi za East Africa lakini hata wananchi wa nchi hizo wanatumia lugha ya Kingeleza kufanya biashara mbali mbali nje ya nchi zao.Sisi watanzania tuko wapi? mbona tunajidanganya.Lugha zote zipewe umuhimu ulio sawa katika kufundishia hapo sawa.
Tujifunze vp tena wakati kiingereza ndio kinatumika kufundishia kwa sasa na ndiyo maana watu wanapinga kubadilisha hivyo na kufundishia kwa kiswahili kwa hoja kwamba tutakuwa hatujui kiingereza,ndiyo nasema kwamba sasa hivi pamoja ya kwamba tunafundishwa kwa kiingereza lakini matokeo kwenye uhalisia watanzania kiingereza hatujui.Ndio tujifunze sasa, kwani hakuna muujiza. Tuna tabia ya uzembe, kitu kikitushinda tunakiharamisha. Kwani yale tunayojifunza kwa Kiswahili hatufeli?
Hao wenye shida ya kuzungumza kiswahili itakuwa labda wahindi na wasomali.Siungi mkono hoja. Kiswahili chenyewe kukizungumza shida je kufundishia. Si itakua shida
Huwezi fanya invention yoyote iwapo umekariri maarifa kwasababu hukuelewa vizuri lugha waliyokufundishia. Kama viongozi na maprof hawajui kiingereza mtoto wa form 1 atajuaje? Hivi kuna ujinga mkubwa zaidi ya kufundisha watu kwa kutumia lugha wasiyoielewa?. Ghafla nikuchukue hapa na kuanza kukufundisha uraia kwa kisandawe!!!!.Hauielewi vizuri sababu tunakuwa kama wapumbafu, primary watoto wanasoma kiswahili, sekondari kwa lugha ya kiingereza, kama sio upunguani kwa watunga Sera ni nini? Hawaoni hii inconsistency ndio unaleta aibu kwa taifa Leo viongozi wanaongea kiingereza kama sio wasomi? Kama wanaona ni sawa mbona wakipata madaraka na vijisenti watoto wa hawa viongozi wanasoma better schools medium of instruction ni kiingereza? Lugha watu wanajifunza, kwann tuhangaike na li lugha LA kiswahili wakati hata inventions hatufanya? Technologies zote tunanunua? Hicho kiswahili hakitusaidii chochote zaidi ya kutuunganisha kama taifa huko mtaani!!
Hii ina maanisha kuwa uwezo wa kufikiri au kutatua jambo hauwezi kuathiriwa na lugha maana lugha hutumika tu huelezea fikra, mawazo na ndoto. Ndiyo maana mabubu na wasiosikia wanaweza kutatua changamoto ktk jamii zao.The statement would come true in a sense when you have speak according to a situation. So I definitely believe a thought comes first. So the language is used to communicate a person's thought. Never the other way around.
Naona haujanielewa, kiingereza ni lugha kama lugha zingine, ili kuielewa vizuri iwe lugha ya kufundishia toka primary school, sio kukutana nayo juu kwa juu secondary, hiyo ndio njia pekee, hauna sababu ya kufundishana kiswahili hata publication za kiswahili tu hamna itabidi tutafsiri publications kibao ambapo huo uwezo hatuna, kiswahili kingebaki kama somo, hao viongozi wenyewe watoto wao hawasomi shule zinazofundisha kiswahili, why? Sababu wanajua ni upuuzi! Mmebaki nyie wanyonge na watoto wenu.Huwezi fanya invention yoyote iwapo umekariri maarifa kwasababu hukuelewa vizuri lugha waliyokufundishia. Kama viongozi na maprof hawajui kiingereza mtoto wa form 1 atajuaje? Hivi kuna ujinga mkubwa zaidi ya kufundisha watu kwa kutumia lugha wasiyoielewa?. Ghafla nikuchukue hapa na kuanza kukufundisha uraia kwa kisandawe!!!!.