Pendekezo: Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu, ili tukomboke kifikra

Pendekezo: Kiswahili kitumike kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu, ili tukomboke kifikra

Hebu nitajie hata maneno 10 ya kilatini ambayo yapo kwa kiswahili.
Achana na China haiwezi kukusaidi kitu, ongelea Taifa lako.
China wamekataa cheo cha kuwa developed ili wapate 'fursa' fulani za kiuchumi. Kwa ulingano ni kwamba vyuo vinavyofundisha kwa kichina ni vingi kuliko kiingereza.

Ishu za kilatini ni misamiati na inatoholewa kwenda kwenye lugha mbali mbali ili kurahisisha uelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi wa binadamu wanaopigia chapuo huu mswada mfu watoto wao wamewapeleka English Medium Schools, hawataki kuwa mfano. Kiingereza ni lugha kubwa, kujifanya tunapenda saana Kiswahili ni kichaka cha kuficha kushindwa kwetu kumudu Kiingereza.

Wachina walianza kuendeleza teknolojia ndogo ndogo za mashambani ndio wakajifungia. Sisi tunaanza na mdomo
Ni kweli hii lugha hatuielewi pamoja na kwamba ndio inayotumika kufundishia wakati huu hivyo hizo faida za kiingereza tunazikosa vilevile.
 
Yaani kwa kuwa jamaa lugha inamgonga ndiyo unaleta pendekezo hilo sasa, hapana. Mtu ni PhD holder halafu simple english inamtoa kamasi inaahangaza .
Sasa hapo ndio pa kujiuliza inakuaje hivyo wakati sasa tunatumia kiingereza kufundishia? Kama kufundishwa kwa kiingereza ndio kunafanya tujue kiingereza sasa mbona wabongo hatujui hicho kiingereza hadi hao wenye PHD bado pia kiingereza kinawapa tabu?
 
Wale wanaotamani Kiswahili iwe lugha yakufundishia mashuleni hawapeleki watoto wao kwenye hizo shule za kiswahili wanawahangaikia kuwapeleka kwenye shule za English Medium.

Haiwezekani ukapuuza lugha ya Ulimwengu kingeleza yaani English ukakazania lugha inayotumika katika nchi yako tu.Hata kama kiswahili kinatumika nchi za East Africa lakini hata wananchi wa nchi hizo wanatumia lugha ya Kingeleza kufanya biashara mbali mbali nje ya nchi zao.

Sisi watanzania tuko wapi? mbona tunajidanganya.Lugha zote zipewe umuhimu ulio sawa katika kufundishia hapo sawa.
 
Ziko faida na pia hasara za kufundisha kwa Kiingereza. Na naongelea kufundisha kwa Kiingereza kuanzia darasa la 3 kama ilivyokuwa ikifanyika hadi 1965. Kipindi hicho mhitimu wa elimu ya msingi alikuwa anafahamu Kiingereza kiasi cha kutosha kusoma vizuri masomo ya sekondari, kwa Kiingereza. Na mhitimu wa kidato cha 4 alikuwa anafanya mitihani ya kuandika na kuzungumza Kiingereza (shule zilikuwa na majopo la kutahini Oral English).

FAIDA ZA KUFUNDISHA KWA KIINGEREZA (kuanzia darasa la 3)
  • Wahitimu wanakuwa na ustadi wa Kiingereza na pia Kiswahili. Kiswahili kinafahamika hata kwa wasiokwenda shule, kwa hivyo si lazima kusoma kwa Kiswahili ili wajue Kiswahili.
  • Sekta ya Utalii ni muhimu sana kwenye uchumi. Lazima tuwe na taifa linalozungumza lugha zinazozoeleka zaidi duniani. Watu kama maofiza wa Uhamiaji, Wanausalama, wafanyakazi viwanja vya ndege, mahospitalini na mahotelini shurti waweze kundika na kuzungumza Kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha, na sio Kiswahili pekee.
  • Nchi husikika zaidi kwenye habari kimataifa kama interviews za kiingereza ni rahisi kufanyika. Utaona kwa sasa mashirika ya habari kama TV za BBC na Aljazeera huwa wanazungumza zaidi na Wakenya, Waganda, Wanajeria na kwingineko amabako Kiingereza kinazungumzwa na watu barabarani. Ni nadra kuwaona wakizungumza na watu kwetu.
  • Tunaelekea ulimwengu ambapo maarifa (knowledge) yote yatapatikana mtanadaoni bure, lakini sehemu kubwa itakuwa ni kwa Kiingereza. Wasiokuwa na ustadi wa kutosha wa Kiingereza watasota sana.
  • Mtanzania mwenye kufahamu vizuri Kiingereza na Kiswahili huwa anajiamini zaidi ya aliye na Kiswahili peke yake.
  • Ajira nyingi ndani na nje ya nchi zinawapita Watanzania kwa kushindwa kwao kuongea na kuandika Kiingereza. Hili tatizo litaondoka kama tukifundihs kwa Kiingereza tangu darasa la 3.
  • Etc. Ziko nyingi. Nitatoa zaidi zikihitajika
HASARA:

Hasara pekee ninayofahamu ni kwamba kwa sasa, kutokana na ufinyu wa uelewa wa Kiingereza, Watoto wanaposoma kwa lugha hiyo kwa kuanzia shule za sekondari hawaelewi vizuri na wanaishia kukariri. Wale wanaosoma kwa Kiingereza toka darasa la kwanza hawana tatizo hili.

SERA. Iwe basi sera ya serikali kuajiri tu wale wanaoweza kuzungumza na kuandika Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha, na sio Kiswahili peke yake. Iwe sera pia kwamba Tanzania ni nchi yenye lugha rasmi mbili, Kiswahili na Kiingereza.
 
Kwani mbona hata sasa wakenya wanatuburuza sana tu kwa kuwa sie hatujui hicho kiingereza?
Ndio tujifunze sasa, kwani hakuna muujiza. Tuna tabia ya uzembe, kitu kikitushinda tunakiharamisha. Kwani yale tunayojifunza kwa Kiswahili hatufeli?
 
Wale wanaotamani Kiswahili iwe lugha yakufundishia mashuleni hawapeleki watoto wao kwenye hizo shule za kiswahili wanawahangaikia kuwapeleka kwenye shule za English Medium.Haiwezekani ukapuuza lugha ya Ulimwengu kingeleza yaani English ukakazania lugha inayotumika katika nchi yako tu.Hata kama kiswahili kinatumika nchi za East Africa lakini hata wananchi wa nchi hizo wanatumia lugha ya Kingeleza kufanya biashara mbali mbali nje ya nchi zao.Sisi watanzania tuko wapi? mbona tunajidanganya.Lugha zote zipewe umuhimu ulio sawa katika kufundishia hapo sawa.
Kumbe watu wanapeleka watoto zao hizo shule ili tu wajue kiingereza na si kwamba wanawapeleka kwa ubora wa elimu! Ndiyo maana kuna baadhi ya watoto unakuta anaongea kiingereza vizuri tu ila kichwani hakuna kitu.
 
Ndio tujifunze sasa, kwani hakuna muujiza. Tuna tabia ya uzembe, kitu kikitushinda tunakiharamisha. Kwani yale tunayojifunza kwa Kiswahili hatufeli?
Tujifunze vp tena wakati kiingereza ndio kinatumika kufundishia kwa sasa na ndiyo maana watu wanapinga kubadilisha hivyo na kufundishia kwa kiswahili kwa hoja kwamba tutakuwa hatujui kiingereza,ndiyo nasema kwamba sasa hivi pamoja ya kwamba tunafundishwa kwa kiingereza lakini matokeo kwenye uhalisia watanzania kiingereza hatujui.
 
Naomba kuuliza,

Tuchukulie ni kweli hicho kiswahili kikaruhusiwa kuwa Lugha ya ufundishiaji

Je tutapata wapi 'contents' za kufundishia huko vyuoni?

Au unataka kutuaminisha kwamba walimu kama kina Dr Bashilu wanauwezo wa kuandaa maudhui ya watoto huko vyuoni?

Tuache utani, suala la Kiswahili kuwa Lugha ya kufundishia bado muda wake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siungi mkono hoja. Kiswahili chenyewe kukizungumza shida je kufundishia. Si itakua shida
 
Tuache siasa Kiswahili bado hakijafikia hatua ya kutumika hadi university mara moja. Tuende taratibu kwa hatua la sivyo tutapoteza ubora wa elimu yetu mara moja
 
Masshele,
Ubunifu hauna lugha wala kukariri kwa kusoma sana. Mfumo maalum wa kuibua na kuendeleza vipaji ili viunganishwe ktk uzalishaji mkubwa kupitia viwanda vya kati na vikubwa ndiyo jibu.

Made in Tanzania by Emmanuel Luvanga



Source : Millard Ayo
 
Kuzaliwa mtu mweusi ni shida chek mawazo mgando yanavyanavyotolewa tena bila uwoga tungekuwa na pesa ningebadili ngozi
 
Hauielewi vizuri sababu tunakuwa kama wapumbafu, primary watoto wanasoma kiswahili, sekondari kwa lugha ya kiingereza, kama sio upunguani kwa watunga Sera ni nini? Hawaoni hii inconsistency ndio unaleta aibu kwa taifa Leo viongozi wanaongea kiingereza kama sio wasomi? Kama wanaona ni sawa mbona wakipata madaraka na vijisenti watoto wa hawa viongozi wanasoma better schools medium of instruction ni kiingereza? Lugha watu wanajifunza, kwann tuhangaike na li lugha LA kiswahili wakati hata inventions hatufanya? Technologies zote tunanunua? Hicho kiswahili hakitusaidii chochote zaidi ya kutuunganisha kama taifa huko mtaani!!
Huwezi fanya invention yoyote iwapo umekariri maarifa kwasababu hukuelewa vizuri lugha waliyokufundishia. Kama viongozi na maprof hawajui kiingereza mtoto wa form 1 atajuaje? Hivi kuna ujinga mkubwa zaidi ya kufundisha watu kwa kutumia lugha wasiyoielewa?. Ghafla nikuchukue hapa na kuanza kukufundisha uraia kwa kisandawe!!!!.
 
Wabobezi wa fikra, saikolijia, ubunifu na uvumbuzi wanasema lugha ni nyenzo kuelezea fikra, mawazo au ndoto lakini kamwe lugha haiwezi kusaidia fikra za kibunifu, mawazo au ndoto.
The statement would come true in a sense when you have speak according to a situation. So I definitely believe a thought comes first. So the language is used to communicate a person's thought. Never the other way around.
Hii ina maanisha kuwa uwezo wa kufikiri au kutatua jambo hauwezi kuathiriwa na lugha maana lugha hutumika tu huelezea fikra, mawazo na ndoto. Ndiyo maana mabubu na wasiosikia wanaweza kutatua changamoto ktk jamii zao.

Tuache kusingizia lugha inatukwamisha kuendelea kama watu, jamii au nchi.
 
MASSHELE,
Kiswahili kinatosha huko huko mtaani kwa kweli kwenye ngazi ya elimu kiswahili sio kabisa hakitasaidia chochote na watu watakuwa mandondocha tu ni muhimu kujifunza lugha mbali mbali za kigeni kuongeza ujuzi zaidi
 
Huwezi fanya invention yoyote iwapo umekariri maarifa kwasababu hukuelewa vizuri lugha waliyokufundishia. Kama viongozi na maprof hawajui kiingereza mtoto wa form 1 atajuaje? Hivi kuna ujinga mkubwa zaidi ya kufundisha watu kwa kutumia lugha wasiyoielewa?. Ghafla nikuchukue hapa na kuanza kukufundisha uraia kwa kisandawe!!!!.
Naona haujanielewa, kiingereza ni lugha kama lugha zingine, ili kuielewa vizuri iwe lugha ya kufundishia toka primary school, sio kukutana nayo juu kwa juu secondary, hiyo ndio njia pekee, hauna sababu ya kufundishana kiswahili hata publication za kiswahili tu hamna itabidi tutafsiri publications kibao ambapo huo uwezo hatuna, kiswahili kingebaki kama somo, hao viongozi wenyewe watoto wao hawasomi shule zinazofundisha kiswahili, why? Sababu wanajua ni upuuzi! Mmebaki nyie wanyonge na watoto wenu.
 
Back
Top Bottom