Pendekezo: Kitengo cha Upelelezi kitolewe Polisi

Ni Kweli kiondolewe.
 
Wazo ni zuri ili polisi wafanye kazi zingine,na kiwe huru kisifungamane na upande wowote ili kuleta haki kwenye jamii.Polisi kuna mapungufu mengi zipo case study za watuhumiwa kulazimishwa kukubali kusainishwa hata kwa makofi na vipigo na watu kulazimishwa kukiri.Kiwe huru kijitegemee kiwe na muundo wake tofauti kiajiri wasomi waliobobea kwenye upelelezi na uchunguzi kuwa chini ya polisi kwakweli si haki kwa maana kuwa chini ya polisi kuna mapungufu mengi sana ya kiutendaji,mfumo na muundo wa polisi umejengwa kwenye matumizi ya nguvu na amri zaidi na si weledi na utu hao wabakie kwenye kazi za kutumia nguvu tu.Upelelezi unataka matumizi makubwa ya akili kuliko nguvu ili kutenda haki haki ikitendeka tutapunguza msongamano wa mahabusu,uchelewaji wa kesi,gharama za kuhudumia mahabusu,itapunguza rushwa maana mahabusu ni miradi ya watu ili kesi yako upelelezi ukamilike haraka ni lzm utoe rushwa kama utaki kukaa mahabusu mda mrefu zaidi ya hapo utaozea utasaulika mahabusu kila siku upelelezi haujakamilika,sasa kama upelelezi haujakamilika mnamshikilia vipi mtu, kwann msikamilishe upelelezi kwanza kisha ndo mmshikilie MTU.
 

Yaani bora hata ungeitaja nchi nyingine hapo tofauti na Rwanda Mkuu kwani hakuna nchi ambayo inachukiwa na Watanzania kama ya Rwanda japo ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania ina mengi ya Kujifunza kwa Rwanda hata kuliko Rwanda ambavyo inaweza Kujifunza kwa Tanzania. Na Kitu kikubwa ambacho Watanzania wanaweza Kujifunza kutoka kwa Taifa la Rwanda na hasa Wanyarwanda ni namna gani ya Kutumia ' Akili ' vizuri katika Kujieletea Maendeleo. Binadamu wote tuna Akili ila Akili za Wanyarwanda zinatumika mahala sahihi na kwa wakati sahihi na pia kwa malengo yaliyo sahihi kabisa. Chuki ya Watanzania kwa Wanyarwanda na Taifa lao la Rwanda wangeigeuza iwe ni Upendo na Imani Kwao basi leo wangekuwa mbali mno na Wanyarwanda siyo Wachoyo wa Kukupa ' Maarifa ' kama wakijua au ukijijua Wewe ni ' Popoma Mwandamizi ' kabisa. Ukiichukia Rwanda na Wanyarwanda ni lazima tu utakuwa na matatizo makubwa ya ' Akili ' na pengine unahitaji Tiba ya haraka Mirembe.

Long live Rwanda!
 
Ofisi ya DPP inapwaya sana inavunja haki za watu tuwe jamii ya watu tulioelimika na kustaarabika ukitembelea mahabusu ni malalamiko tu watu wanakaa miaka kila siku upelelezi haujakamilika kwann msikamilishe upelelezi kwanza kisha ndo mmshikilie mtu,tungekuwa na utaratibu wa watendaji kuanzia wakamataji,waendesha mashtaka,ofisi ya mwanasheria mkuu nk kukatwa mishahara yao ili ikatumike kulipa fidia watuhumiwa waliokaa mda mrefu mahabusu na kuachiliwa bila ushahidi zitumike kuwalipa fidia ingesaidia sana kuondoa uzembe huu wa kuchezea maisha ya watu.Pia mtuhumiwa akishikiliwa mahabusu hukumu ya kifungo ikitoka siku ziheshabiwe kuanzia zile alizotumikia mahabusu. MTU anakaa mahabusu miaka 7 kisha unamfunga miaka 7 hii si jumla ni miaka 14 sasa.Hivi nyie watunga na wasimamizi wa sheria mahakimu,wanasheria,waendesha mashataka,nk nyumba za ibada huwa mnaenda kufanya nn kuwajazia waumini wa kweli viti,kusali kwenu ni bure,hizo sheria sio msahafu zisibadilike kuendana na nyakati tufanye mambo kama jamii ya watu walioelimika watu walioelimika ustaarabika,maana jela na hospital ni mtakuja hapana mwenyewe yeyeto anawezaingia bila kujali ni kiongozi au muongozwa,tunapokuwa na nafasi ya kuweka mazingira bora tuyaweke sasa sio unafika jela ndo unatamani kuyaweka wakati huo huna nafasi tena mfumo umekutupa.Tusiwe kama Dikteta Bashiru wa Sudan kulalamikia hali ya gereza alilowekwa kuwa ni baya baada ya kuwekwa humo.Siku zaja nany mtajikuta magerezani amini nawaambieni.
 
Tungeanza Kwanza nakubadili mfumo wa jeshi letu la Polisi.Liitwe TANZANIA POLICE SERVICE.
 
Waongopee wasiojua Rwanda,kuna maendeleo gani,au maghorofa ndio maendeleo. Alichoweza MTU mrefu ni kuzuia mabaya ya nchi yake yasitoke nje kwa kufanikiwa kuchuja habari azitakazo yeye ndo zitoke ukiripoti kinyume lzm usione kesho yako anasema umevuka mstari mwekundu.Subiri akiondoka madaraka si umilele hata kwa uzee haukimbiwi yataibuliwa mabaya.Rwanda si mfano mzuri wa haki za binadamu hasa watuhumiwa kusingekuwepo na mrundikano wa mahabusu magereza ya Rwanda.
 
Tungeanza Kwanza nakubadili mfumo wa jeshi letu la Polisi.Liitwe TANZANIA POLICE SERVICE.
Aliweza IGP Msomi Said Mwema Mungu ampe maisha marefu kwa kulifanya jeshi kiwe services angalau liwe kisomi zaidi.
 
Ni kweli mkuu

Kuna baadhi ya kesi hubambikwa na hao hao polisi halafu wao wao wanapeleleza

Yani mbuzi anafia kwa muuza supu what do you expect
 
TIA - (TANZANIA INTELLIGENCE AGENCY)
Is coming soon [emoji4][emoji4][emoji4]

Asante sana Mheshimiwa Rais kwa kuliona hili.
 

Just keep your ' Pig Mouth ' shut please!
 
Hata ikitengwa,,watumishi wake pia waharifu watakuepo

Ni kama ilivyo TAKUKURU pia inawafanyakazi wala rushwa
Ishu siyo kwamba nako watakuwepo. Investigation zilizo nyingi zinahitaji professionalism.
 
Upelelezi unaozungumziwa hapa ni cases kama zile mtu amepata ajali ameharibu labda mali za watu. Hivyo mwenye mali zake labda akaenda kufungua kesi.
 
Kitolewe kwasababu zipi?
Weka sababu na sio kuleta maada za kutaka jambo lifanyike kwa manufaa au chuki zako au kwa kuiga
Upelelezi unahitaji professionalism siyo porojo.
 
logic
 
Tungeanza Kwanza nakubadili mfumo wa jeshi letu la Polisi.Liitwe TANZANIA POLICE SERVICE.
Hili nalo ni neon mkuu,halafu tungeunda IPID hawa ni polisi wa kuwachunguza polisi kuona wanaendesha shughuli zao kwa kufuata sharia,wana uwezo wa to arrest police mwenzao,wana uwezo wa kupeleleza kesi inayowahusu polisi na wana uwezo wa kumpeleka mahakamani polisi anayeonekana ana kesi ya kujibu;kwa Tanzania tunatusubiria sana.
 
Upepelezi unahitaji professionalism. Hivyo kuwaachia hilo jukumu polisi siyo sawa kabisa.
True polisi ni matumizi ya nguvu zaidi kuliko akili we check hata ukienda mapokezi zao si professionalism kabisa mnatreatiwa kwa ukali ukali tu.Nature ya kazi zao ndo inawashape hivo wapelelezi wasichanganywe wawe huru ili wasipate ile inayoitwa police culture, wawe huru kufanya kazi professionalism kama FBI,CIA,nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…