mzee kama hujui ungeuliza, ndani ya nchi yetu kuna vikosi vingi vya dhahiri na vya siri, ukiwa nje kwa jicho la kawaida huwezi kuvigundua, kwa kifupi upelelezi umeanzia mbali sana, kuna boda boda, washona viatu, wafanyabiashara ndogo ndogo, waganga wa kienyeji, mabalozi wa mitaa, mabarozi wa vijiji, wahudumu wa baa, watangazaji, waandishi wa habari, mapolisi, wanajeshi, askri magereza, zimamoto, uhamiaji, mgambo nk. n.k.... ila sijasema kuwa wote nilio wataja hapo ni wapelelezi ila ndani ya hayo makundi kuna wapelelezi ambao sio polisi ila nao ni wapelelezi wenye malengo tofauti tofauti kutokana na mahitaji husika.
kikosi cha INTELIJENSIA ndani ya jeshi la polisi kimefanya kazi kubwa, na kitaendelea kufanya kazi nzuri, hakitaondolewa kama unavyodhani isipokuwa kitazidi kuimarishwa ili waweze kupambana na majanga ambayo unadhani wameshindwa kufanya.