Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 10,488
- 20,051
Salamu Wakuu wa JF
SSH 25 30
Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ni wazi kuwa ushindani wa kisiasa unazidi kuwa wa kisasa na unaotegemea zaidi teknolojia na mawasiliano ya umma. Kwa kuzingatia hali hiyo, chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinashauriwa kuangalia uwezekano wa kuanzisha au kununua chaneli ya televisheni ya ndani ambayo itakuwa maalum kwa ajili ya kueneza ajenda, sera, mafanikio, na malengo ya chama kwa wananchi.
Tukiweka mbali ya Taifa nadhani itafanya kazi vizuri sana chaneli binafsi ya televisheni ikapatikana kwenye vyombo vya umma kama mabasi yaendayo mikoani. Hapa chama kiangalie namna yakuingia ubia na wamiliki wa haya mabasi akubwa ya abiria na hata mabasi ya kati maarufu (kosta) zikafungwa ving'amuzi inapopatikana hiyo chaneli.
Fikiria mtanzania asafiri kwa saa zisizopungua 9 kutoka Dar es Salaam hadi Arusha yeye anaangalia na kusikia habari za chama chetu tu. Kutoka kila jimbo kila kona ya nchi. Hapa lazima tutapata kuongeza ushawishi zaidi na zaidi. Hata ajira kwa vijana maripota wapya waliotoka vyuo zitapatikana
Faida za Mkakati huu:-
1. Ufikaji wa Moja kwa Moja kwa Wananchi: Kupitia chaneli hiyo, CCM inaweza kufikisha ujumbe wake moja kwa moja kwa wananchi bila mabadiliko au upotoshaji wa taarifa. Yaani mtanzania anaona kabisa na kuzisikia mubashara sera za wagombea ubunge, udiwani na ngazi ya uraisi pale kwa mama daktari Mh. Samia Suluhu Hassan. Hapa na simu ziweze kupigwa na wananchi zikasikika mubashara juu ya waonavyo wao na maoni pia. Tusiogope simu za kukosoa na maswali tata sababu nina imani tupo na wagombea wanaoweza kujieleza na kufafanua sera na ilani yetu kwa ujumla.
2. Elimu ya Mpiga Kura: Televisheni hiyo inaweza kutumika kuelimisha wananchi kuhusu haki zao za kidemokrasia, namna ya kupiga kura, na umuhimu wa ushiriki wa kisiasa kwa amani. Hapa hata mataifa ya nje na waangalizi wa kimataifa hawatakuwa na wasiwasi wala kuuliza juu ya ushindi wowote ule maana kazi wataiona ilivyotendeka
3. Ushiriki wa Vijijini: Kwa kuweka chaneli hii ipatikane kwenye mabasi yaendayo mikoani, maeneo ya vijijini, na vituo vya huduma za jamii, chama kinaweza kuwafikia wananchi wengi zaidi walioko nje ya miji mikuu. Kwenye vijiji huko tuweke luninga japo moja moja kwenye maeneo ya mikusanyiko yaliyo maarufu watu wasikilize na waone sera zetu mubashara. Hapa tutaweza kwenda sawa na udogo wa masaa ya kufanya kampeni kwani sisi tutakuwepo hadi kwenye malininga muda wore.
4. Maudhui Mbalimbali: Kituo hiki kinaweza kuwa na vipindi vya mahojiano, filamu za uhamasishaji, muziki wa kizalendo, na midahalo ya sera ili kuimarisha uelewa wa wananchi.
Uzingatiaji wa Kisheria:
Ni muhimu kuhakikisha kituo hicho kinafuata masharti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kinakuwa na usajili halali, na hakitumiwi kuchochea vurugu wala chuki. Pia, ni vyema kuwa na uwiano wa kuruhusu mijadala ya hoja mbalimbali za kitaifa kwa njia ya heshima. Hapa tutaweza pia kujibu lile swali la muda wate kuwa muda ni mchache tufanyaje?.
Hitimisho:
Katika ulimwengu wa leo, mawasiliano ni silaha kuu ya kisiasa. CCM ikiwa chama kilicho na historia ndefu ya siasa za amani, kina nafasi ya kutumia vyombo vya habari vya umiliki wake kama nyenzo ya kuimarisha mawasiliano na wananchi na kuendeleza ajenda zake kuelekea maendeleo ya taifa.
Kazi na Utu, Tunasonga mbele.